Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UCHAGUZI-SIASA

Kaboré achaguliwa kuwa rais wa Burkina Faso katika duru ya kwanza

Mgombea urais nchini, Zéphirin Diabré amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Roch Marc Christian Kaboré.

Roch Marc Mkristo Kaboré, kwenye makao makuu ya chama chake tarehe 1 Desemba 2015, kufuatia tangazo la ushindi wake katika uchaguzi wa rais nchini Burkina Faso.
Roch Marc Mkristo Kaboré, kwenye makao makuu ya chama chake tarehe 1 Desemba 2015, kufuatia tangazo la ushindi wake katika uchaguzi wa rais nchini Burkina Faso. © AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama cha MPP ameshinda uchaguzi huu wa kihistoria wa urais katika duru ya kwanza kwa 53.49% ya kura dhidi ya 29.65% ya mgombea wa chama cha UPC, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI).

Hali hiyo imeibuka usiku wa manane katika makao makuu ya chama cha UPC, chama cha Zéphirin Diabré, wakati mgombea huyo alijitokeza na kutangaza kwa waandishi wa habari kwamba anaelekea kwa mpinzani wake, kwenye makao makuu ya chama cha MPP cha Roch Marc Mkristo Kaboré, ili kumpongeza kwa ushindi wake, kifikra na katika makubaliano mazuri.

Aliwasili mnamo saa 7:00 usiku kwenye makao makuu ya mpinzani wake katika hali ya kushangaza, ambapo alizungumza na mshindi wa uchaguzi huo wa urais. Zéphirin Diabré, katika ishara ya heshima, alikubali mara moja kushindwa na kumalizika mashaka. "Hakuna kupingwa kwa uchaguzi huu", Zéphirin Diabré alisema.

Akipongezwa na maelfu ya watu waliokusanyika nje ya makao makuu ya chama chake, Bw Kaboré aliwaambia wafuasi wafuasi wake: "Tunapaswa kuanza kazi haraka iwezekanavyo. Ni sote pamoja tunapaswa kutumikia nchi". Rais mpya aliyechaguliwa pia aliwaahidi raia wa Burkina Faso "uamuzi wake wa kufungua fursa bora kwa siku zijazo", huku akipongeza "taasisi za mpito" ziliyowekwa baada ya kuangushwa utawala wa Compaoré na ambazo ziliandaa uchaguzi.

CENI imetoa matokeo ya awali ya uchaguzi: 53.49% (sawa na kura 1,668,169) ndizo alizipata Bw. Kaboré dhidi 29.65% (sawa na kura 924,811) za Bw. Diabré. Roch Marc Christian Kaboré amepata ushindi katika uchaguzi huo wa kihistoria katika duru ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.