Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Tanzania: NEC mbioni kutoa daftari la kudumu la wapiga kura

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania, NEC, imesema kuwa inatarajia kutoa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa na kubandikwa katika vituo vya kupigia kura kwa lengo la kuwawezesha wapiga kura na vyama vya siasa kuhakiki wapiga.

Dar es Salaam, kunakopatikana makao makuu ya Tume ya uchaguzi nchini Tanzania.
Dar es Salaam, kunakopatikana makao makuu ya Tume ya uchaguzi nchini Tanzania. Getty Images/Ariadne Van Zandbergen
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imefikiwa na tume baada ya majuma kadhaa yaliyopita, wanaharakati na vyama vya siasa kulalama kuhusu tume kuchelewesha daftari hilo kwa hofu kuwa huenda muda ungekuwa mdogo kwa wananchi na vyama kuhakiki wapiga kura.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na rfikiswahili, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania, jaji mstaafu Damian Lubuva, amewaondoa hofu wananchi na vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Kuwekwa wazi kwa daftari la kudumu la wapiga kura, sasa kutawawezesha wananchi kuhakiki majina yao na kutambua idadi rasmi ya wapiga kura walioandikishwa kwenye vituo vya kupigia kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.