Pata taarifa kuu
BURUNDI-MATESO-MAUAJI-USALAMA

Hati za kukamatwa zatolewa dhidi ya wapinzani: wasi wasi mkubwa Burundi

Nchini Burundi Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa Valentin Bagorikunda, ametangaza Ijumaa wiki hii kwamba Ofisi yake imetoa hati za kikamataifa za kukamatwa dhidi viongozi wa “ harakazi za kupinga muhula wa tatu ” wa Rais Pierre Nkurunziza, ikiwa ni pamoja na vyama vya kisiasa, vyama vya kiraia pamoja na vyombo vya habari binafsi.

Askari polisi akipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai.
Askari polisi akipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Vyote hivyo vinatuhumiwa kuanzisha kundi la uasi nchini na kula njama za jiribio la mapinduzi dhidi ya Pierre Nkurunziza lililotibuka Mei 13 mwaka 2015. Valentin Bagorikunda amesema hayo kulingana na ripoti ya kamati ya uchunguzi iliyoteuliwa na Ofisi ya mashtaka ili kuendesha uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi lililotibuka. Rfi ilipata kopi ya ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ilitaja majina ya wapinzani wakuu na wanaharakati muhimu wa mashirika ya kiraia. Jean Minani, kiongozi wa chama cha Frodebu-Nyakuri, ambaye aliwahi kuwa mara mbili Spika wa Bunge ni miongoni mwa watu hao waliotajwa.

Jean Minani ametupilia mbali ripoti hiyo ya Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa akibaini kwamba hawajibiki katika kazi yake. “ Watu wanauawa hadharani, watu wakishuhudia, Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa hasemi lolote... Miili ya watu waliouawa inagunduliwa hapa na pale nchini, maiti zinaokotwa zikiwa zimefungwa kamba, baada ya kukamatwa na polisi, kila mtu anafahamu wanaotenda maovu hayo, lakini Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa hasemi lolote wala kukataza maovu hayo. Watu wanafanyiwa mateso ya aina mbalimbali hadi wanauawa, Mwendesha mashtaka hasemi lolote ”, amelaani Jean Minani.

Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha Frodebu-Nyakuri, Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa anautuhumu upinzani kwa kila maovu yanayotendwa nchi Burundi. “ Hiyo inamaanisha kuwa Mwendesha mashtaka mkuu hafai kuwa Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa na amekua sasa mfuasi wa Pierre Nkurunziza. Kwa hiyo tunasema hakuna aliyeshinda vita dhidi ya raia. Kila siku raia ndio hupata ushindi ”, ameongeza Jean Minani.

Kwa upande wake Innocent Muhozi, hakuna serikali Burundi

Vyombo vya habari binafsi na viongozi wao - wenyewe - walikuwa bado hawajatajwa na hata hivyo mwendesha alivituhumu kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliotibuka. Kwa upande wake Innocent Muhozi, kiongozi wa shirika linalochunguza taaluma ya uandishi wa habari nchini Burundi (OPB), na mkurugenzi wa redio na televisheni Renaissance FM, amesema tangazo hilo la Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa nchini Burundi ni mwendelezo ulio dhahiri wa ukandamizaji wa vyombo vya habari.

" Huu ni muendelezo wa kisiasa ambao unaendelea tangu miaka kadhaa iliyopita, utawala ukijaribu kukandamiza uhuru wa raia na haki ya kiraia. Mashtaka au mauaji ya jinai, kila mtu ana wasiwasi nchini Burundi ambapo inaonekana kuwa hakuna serikali wala taasisi yoyote halali, unapoona hali inavyoendelea kila kukicha nchini humo; mauaji, mauaji ya wafungwa, mateso ... Maovu yote hayo yanatekelezwa na Idara zinazodaiwa kuwa ni za serikali. Kwa upande wetu hali mbaya zaidi yaweza kutokea...", amesema Innocent Muhozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.