Pata taarifa kuu
NIGERIA-CHAD-CAMEROON-BOKO HARAM-Usalama

Majeshi ya Chad yafanikiwa katika operesheni yake

Wanajeshi wa Chad wamefanikiwa kudhibiti mji wa Gamboru, kaskazini mwa Nigeria, baada ya mji huo kutekwa na wanamgambo wa Boko Haram.

Helikopta ya jeshi la Chad ikitua karibu na mji wa Gamboru, Februari 1 mwaka 2015.
Helikopta ya jeshi la Chad ikitua karibu na mji wa Gamboru, Februari 1 mwaka 2015. AFP PHOTO / STEPHANE YAS
Matangazo ya kibiashara

Wanejeshi wa Chad zaidi ya elfu mbili walivuka mpaka wakitokea nchini Cameroon kuja kusaidiana na wale wa Nigeria kupambana na kundi hilo ambalo linaendelea kuwa tishio la usalama kwa ukanda wa Afrika Magharibi.

Maafisa wakuu wa jeshi la Chad wamethibitisha kuwa vikosi vya majeshi yao vimeingia nchini Nigeria kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram.

Msemaji wa idara ya usalama nchini Nigeria, Mike Omeri, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa mapigano yalilenga eneo la kaskazini mashariki mwa mji wa Gamboru, linaloshuhudia mara kwa mara mashambulizi yanayotekelezwa na kundi hilo la kigaidi.

Wachambuzi wanasema kundi hili la Boko Haram limechukuliwa na jumuia ya kimataifa kuwa tishio la usalama wa kikanda.

Maafisa wa usalama nchini Nigeria wanasema kiongozi wa kundi la Boko Haram, Aboubakar Shekau ametishia kuanzisha matawi ya wanamgambo katika maeneo mengine nchini Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Umoja wa Afrika una mpango wa kuunda kikosi cha wanajeshi 7,500 kupambana na Boko Haram.

Wakati hayo yakijiri, kampeni za urais kati ya rais wa sasa Goodluck Jonathan na mpinzani wake Muhamadu Buhari zinaendelea kushika kasi.

Wananchi wa Nigeria watapiga kura tarehe 14 kumchagua kiongozi wao, na wagombea hao wawili wamekuwa wakishtumiana hadharini kwa lengo la kuwavutia wapiga kura.

Rais Jonathan amemwelezea mpinzani wake Muhamadu Buhari kama mtu anayewahurumia wapiganaji wa Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.