Pata taarifa kuu
MOROCCO-UFARANSA-DIPLOMASIA

Salaheddine Mezouar aahirisha ziara yake Ufaransa

Waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Salaheddine Mezouar, ambaye alikua akisubiriwa kuwasili nchini Ufaransa Januari 23 mwaka 2015, katika ziara ya kikazi, ameamua kuahirisha ziara yake kwa tarehe isiyojulikana. Hakuna sababu ziliyotolewa kuhusu kuahirishwa kwa ziara hiyo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Salaheddine Mezouar na Ufaransa Laurent Fabius katika mji wa Rabat, Novemba 14 mwaka 2013.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Salaheddine Mezouar na Ufaransa Laurent Fabius katika mji wa Rabat, Novemba 14 mwaka 2013. AFP PHOTO /FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Lakini vyombo vya habari vya Morocco vinaamini kwamba ukosefu wa maendeleo katika mazungumzo kati ya nchi hizi mbili, uliojitokeza kwa kipindi cha karibu mwaka mmoja sasa, inaweza kuwa moja ya sababu za ya mabadiliko ya ziara hiyo.

Upande wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, wanabaini kwamba serikali ya Ufaransa na Morocco “ zinashirikiana kwa pamoja kwa kuandaa siku nyingine” ambayo itafanyika ziara hiyo iliyoahirishwa.

Waziri wa Ufaransa mwenye dhamana ya mambo ya nje, amesema Waziri wa Morocco anakaribishwa nchini Ufaransa.

Hata hivyo kiukweli ni kwamba uhusiano si mzuri kati ya nchi hizi mbili tangu mwezi Februari mwaka 2014, wakati ambapo polisi ya Ufaransa ilimkabidhi hati ya kutafutwa tajiri mmoja raia wa Morocco, Abdellatif Hammouchi, ambaye alikuwa ziarani mjini Paris. Hati ambayo ilitolewa kufuatia kufunguliwa kwa mashitaka kwa raia wa Morocco walishio Ufaransa.

Tangu wakati huo, mdororo wa kidiplomasia uliendelea kushuhudiwa, na hali hiyo iliendelea kushika kasi baada ya Paris na Algiers kuimarisha ushirikiano wao tangu uchaguzi wa François Hollande. Hali hiyo imesababisha kuvunjika kwa uhusiano katika sekta ya sheria kwa miezi kadhaa sasa, na ushirikiano wa kiusalama pia umedorora, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa.

Huenda ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Morocco ilikua na lengo la kufufua uhusiano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.