Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-Maandamano

Wabunge watazamiwa kutoa heshima kwa waathirika

Rais wa Ufaransa François Hollande, ameongoza sherehe kwenye makao makuu ya polisi mjini Paris mapema Jumanne Januari 13 na heshima ya kitaifa zitatolewa na Wabunge leo mchana.

Bunge la Ufaransa.
Bunge la Ufaransa. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Maisha ya kisiasa yanaonekana kuanza kama kawaida baada ya umoja wa kitaifa kuonekana siku za hivi karibuni. Hata hivyo shambulio la wiki iliyopita bado limo akilini mwa raia wengi wa Ufaransa.

Bunge la Ufaransa linatazamiwa Jumatatu Januari 13 jioni kupitisha uamzi wa kuliongeza muda jeshi la Ufaransa kuendelea na mashambulizi dhidi ya kundi la Doala la Kiislam nchini Iraq.

Wabunge wamekubaliana kuhusu kura hiyo. Uchunguzi wa tume ya bunge kuhusu mtandao wa wanajihadi ambao waziri wa mambo ya ndani alikua anatazamiwa kueleza leo, lakini mkutano huo umeahirishwa.

Kikao cha kawaida cha Jumanne mchana cha maswali kwa serikali kimeahirishwa na muda huo itafanyika sherhe ya kutoa heshima ya kitaifa kwa waathirika wa ugaidi. Waziri mkuu, Manuel Valls atazungumza, hotuba yake ya kwanza baada ya mashambulizi ya wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.