Pata taarifa kuu
CAMEROON-BOKO HARAM-Usalama

Boko Haram yapata pigo kubwa Cameroon

Viongozi wa juu wa Cameroon wamesema kuwa Boko haram imepata pigo kubwa wakati wapiganaji wake walipojaribu kuishambulia ngome moja ya wanajeshi wa cameroon Jana Jumatatu Janauari 12 katika jimbo la Kolofata, Kaskazini mwa cameroon.

Inaonekana mashambulizi ya Boko Haram yameongezeka kwenye mpaka kati ya Cameroon na Nigeria.
Inaonekana mashambulizi ya Boko Haram yameongezeka kwenye mpaka kati ya Cameroon na Nigeria. AFP PHOTO/REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa serikali ya cameroon, jeshi limefaulu kuwaua wapiganaji 143 wa Boko Haram, huku mwanajeshi mmoja wa serikali akipoteza maisha.

Serikali ya Cameroon imeendelea kusema kwamba imefaulu kukamata silaha nyingi za wapiganaji hao na vifaa vingine vya jeshi.

Waziri wa mawasiliano ambaye alitia saini kwenye tangazo hilo la serikali amebaini kwamba ni kwa mara ya kwanza Boko Haram inapateza idadi kubwa ya wapiganaji wake katika mapigano na jeshi la serikali ya Cameroon tangu kundi hilo lilipoanzisha mashambulizi yake nchini humo.

Mapigano hayo yalidumu kwa muda wa saa tano, kabla ya wapiganaji wa Boko Haram kurejea nyuma kufuatia kipigo walichokipata. Baadhi ya picha na video za mapigano hayo zimewekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Jeshi la cameroon limesema kwamba limepoteza mwanajeshi mmoja na wengine wanne ambao walijeruhiwa.

Hii ni mara ya tatu mji wa Kolofata unashambuliwa tangu mwezi Julai mwaka 2014. Shambulio la mwisho kabla ya hili la jana Jumatatu, lilitokea Jumatatu Januari 5 mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.