Pata taarifa kuu
CAMEROON-NIGERIA-BOKO HARAM--Usalama

Raia wa Nigeria wajisikia kutelekezwa katika vita dhidi ya Boko Haram

Baada ya shambulio dhidi ya kambi moja ya jeshi la Cameroon, kaskazini mwa nchi, Jumatatu Januari 12, raia wa Cameroon wanahisi kwamba wamesusiwa na jumuiya ya kimataifa.

Askari wa Cameroon tarehe 17 Juni mwaka 2014, wanapiga doria katika mji wa mpakani wa Amchide, kaskazini ya mwa nchi, mji ambao unakabiliwa na mauaji yanayoendeshwa na Boko Haram.
Askari wa Cameroon tarehe 17 Juni mwaka 2014, wanapiga doria katika mji wa mpakani wa Amchide, kaskazini ya mwa nchi, mji ambao unakabiliwa na mauaji yanayoendeshwa na Boko Haram. Reinnier KAZE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata wanajeshi wa Cameroon, licha ya kupata ushindi katika shambulio la hivi karibuni, wanaona kuwa wanaendesha mapigano hayo pekee yao dhidi ya kundi la Boko Haram, ambalo limeamua kuendelea na mashambulizi katika maeneo ya nchi hiyo.

Juma lililopita, kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau, amewahidi viongozi wa Cameroon kwamba kundi hilo litaongeza mashambulizi yake dhidi ya jeshi la Cameroon.

“ Tunajihisi kwamba tumeachwa pekee yetu katika uwanja wa vita”, msemaji wa jeshi la Cameroon ameelezea masikitiko yake, huku akinyooshea kidole cha lawama Nigeria ambayo haitaki kutoa ushiriki wao katika vita hivyo dhidi ya Boko Haram.

Akihojiwa na RFI, kanali Didier Badjeck, msemaji wa jeshi la Cameroon, amesema anasubiri uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa raia wa Cameroon, ni jambo lisiloeleweka kuona Nigeria ilibani kwamba itapambana na kundi la Boko Haram, lakini imekua ikiwapa nafasi wapiganaji wa Boko Haram kuendelea na mashambulizi kwenye mpaka wa Camerron.

Hata hivyo taratibu za jeshi la cameroon ni kutetea hatua kubwa dhidi ya Boko Haram, hii ikimaanisha kuwa hatua dhidi ya makao makuu ya kundi hilo ikiwa ni pamoja na msitu wa Sambissa, ngome halisi ya Boko Haram katika jimbo la Borno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.