Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria yakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi

Wanawake wawili wamejitoa muhanga kwa kujilipua takriban watu wanne wameuawa kwenye shambulio hilo na zaidi ya arobaini wamejeruhiwa.

Jimbo la Yobe
Jimbo la Yobe DR
Matangazo ya kibiashara

Siku ya jumamosi mwanamke mmoja alijipua kwa bomu mjini Maiduguri kaskazini mwa Nigeria na kuua watu 19.

Mashambulizi haya yamefanyika baada ya kutolewa ripoti kuwa mamia ya watu wameuawa wiki iliyopita katika mji uliokuwa ukishikiliwa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno.

Hayo yanajiri wakati jeshi la Nigeria limeomba msaada wa kupambana na kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi kubwa lililotokea katika mji mmoja wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na ambalo linahofiwa kuwa ndilo baya zaidi kuwahi kufanyika katika uasi wa kundi hilo uliodumu miaka sita sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.