Pata taarifa kuu
NIGERIA-CHAD-NIGER-BOKO HARAM-Usalama

Boko Haram yaiteka kambi ya jeshi

Tangu Jumamosi Januari 3 mwaka 2015 asubuhi, kundi la Boko Haram inaidhibiti kambi ya kikosi cha wanajeshi wakimataifa katika mji wa Baga, kilomita chache kutoka Ziwa Chad.

Wanajeshi wa Nigeria katika mitaa ya mji wa Baga, katika jimbo la Borno, mwezi Aprili mwaka 2013.
Wanajeshi wa Nigeria katika mitaa ya mji wa Baga, katika jimbo la Borno, mwezi Aprili mwaka 2013. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Askari wa Nigeria ambao walikua pekee yao katika eneo hilo walitimka wakati kambi hiyo iliposhambuliwa.

Baada ya kuchukua udhibiti wa kambi hiyo, kundi la Boko Haram lilishambulia vijiji kadhaa vilivyo pembezoni mwa eneo hilo, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya kumi na tano, kama alivyoeleza Seneta kutoka Jimbo la Borno Kaskazini, Maina Ma'aji Lawan, alipohojiwa na RFI.

" Wapiganaji wa Boko Haram walishambulia kambi ya kikosi cha wanajeshi wa kimataifa katika eneo la Baga Jumamosi Januari 3 mwaka 2015. Na jioni, wapiganaji hao walikua wameshakuwa na udhibiti wa kambi hiyo, kwa sababu askari waliondoka katika eneo hilo. Baadaye wapiganaji hao walielea katika mji wa Baga, ambapo waliendesha pia mashambulizi na kisha waliendelea hadi Doron Baga, ambapo pia walipora na kuteka baadhi ya wakazi wa kijiji hicho”, amesema Lawan.

Kwa mujibu wa Senata Maina Ma'aji Lawan, hali hii haieleweki. Baada ya mkutano uliofanyika mjini Paris mwisho wa mwezi Mei, na wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, nchi za ukanda huu ziliahidi kuongeza idadi ya askari, kuimarisha usalama wa kijeshi na kuanzisha vita dhidi ya Boko Haram, lakini nchi hizo ziliamua tu kulinda mipaka yao, amesema seneta kutoka Nigeria Maina Ma'aji Lawan.

" Tulikuwa na idadi ndogo ya askari katika eneo la Baga, walikuwa katika mazingira magumu, kwa wao kuendelea kukaa huko", amesema Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria, Mohamed Bazoum.

Majeshi ya Nigeria na Chad yaliondoka eneo hilo yapata sasa zaidi ya mwezi mmoja. Hata hivyo kila nchi mwanachama wa Tume ya Bonde ya Ziwa Chad (LCBC) ilikuwa imeahidi kutuma kikosi cha wanajeshi wake kujiunga katika kikosi cha kimataifa, ameendelea kusema Mohamed Bazoum.

Raia wa maeneo hayo wameingiliwa na wasiwasi ya kushambuliwa na Boko Haram, na hawajui wapi wakimbilie.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.