Pata taarifa kuu
RWANDA-KIZITO-SHERIA-HAKI

Kifungo cha maisha dhidi ya mwimbaji Kizito Mihigo

Ofisi ya mashitaka imemuombea kifungo cha maisha jela mwimbaji mashuhuri nchini Rwanda, Kizito Mihigo anaeshitakiwa na vyombo vya sheria kwa kupanga njama dhidi ya serikali au rais wa Rwanda.

Kizito Mihigo akiongea mbele ya vyombo vya habari mjini Kigali Aprili 15 mwaka 2014, baada ya tangazo la kukamatwa kwake.
Kizito Mihigo akiongea mbele ya vyombo vya habari mjini Kigali Aprili 15 mwaka 2014, baada ya tangazo la kukamatwa kwake. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Kizito Mihigo anatuhumiwa kosa hilo pamoja na watu wengine watatu akiwemo mwaandishi wa habari.

Muda mrefu akiwa karibu na rais Kagame, Kizito Mihigo sasa anashutumiwa kujiunga na nadharia ya RNC, chama cha upinzani kinachoundwa na baadhi ya wafuasi na viongozi vigogo wa zamani kutoka chama tawala.

Mwezi Aprili uliyopita, kitendo cha kumteka nyara usiku wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari kiliibua hali ya taharuki nchini Rwanda.

Kizito Mihigo, mwimbaji, mtunzi wa muziki, na mmoja kati ya manusura wa mauaji ya kimbari alikamatwa kwa tuhuma za kupanga mashambulizi ya gruneti pamoja na kupanga njama dhidi ya serikali ya Rwanda.

Akizungukwa na polisi, mbele ya vyombo vya habari, Kizito Mihigo alikubali kuwa aliwahi kuwasiliana na uongozi wa RNC, chama cha upinzani ambacho kinaendesha harakati zake kikiwa uhamishoni pamoja na kundi la waasi la FDLR. Kizito aliposikilizwa kwa mara ya kwanza Mahakamani, alikiri makosa yote hayo.

Ofisi ya mashtaka inamtuhumu Kizito Mihigo kuandaa orodha ya watu wanaotakiwa kuuawa, ikiwa ni pamoja na rais Paul Kagame.

Kizito Mihigo alimpoteza baba yake katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Tangu wakati huo, amekua akiimba nyimbo za amani na maridhiano kati ya Wanyarwanda. Jana Jumatatu, baada ya ombi la mwendesha mashitaka, mwimbaji huyo, ambaye hivi karibuni aliwatimua wanasheria wake, aliomba msamaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.