Pata taarifa kuu
MAURITANIA-UISLAM-KUNYONGWA-HAKI-SHERIA

Kijana wa Mauritania ahukumiwa adhabu ya kifo

Kaskazini magharibi mwa Mauritania, kijana mmoja amehukumiwa adhabu ya kifo Alhamisi Desemba 25 kwa kuchapisha habari iliyoonekana kuwa inaukashifu Uislam.

Maandamano ya watu wenye hasira yalifanyika katika mji wa Nouakchott. baadhi ya waandamanaji waliomba Mohamed Ould Mohamed auawe, wakidai kuwa "alikufuru".
Maandamano ya watu wenye hasira yalifanyika katika mji wa Nouakchott. baadhi ya waandamanaji waliomba Mohamed Ould Mohamed auawe, wakidai kuwa "alikufuru". Getty Images/Bernard Foubert
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Cheikh Ould Mohamed alikamatwa Januari 2 mwaka 2014 na kuzuiliwa tangu wakati huo.

Moja ya habari aliyochapisha na kurusha kwenye mitandao ya nchini Mauritania imekua ikilani utaratibu wa jamii nchini Mauritania na kujaribu kuelewa jinsi mafundisho ya Mtume wa mwisho kwa waislam Muhammad yalivyomshawishi.

Watu wengi nchini Mauritania walighadhabishwa na ukosoaji huo, ambao wengi waliona kuwa kijana huyo alimkejeli Mtume Muhammad na kupuuzia Kitabu Kitukufu cha Qurani.

Siku moja baada ya kukamatwa kwake, mfanyabiashara na mhubiri wa mji wa Nouadhibou alikwenda mbali hadi kupendekeza jumla ya Euro 4,000 kwa yeyote atakayemuua Mohamed Ould Cheikh Mohamed.

Hata wakati wa maandamano ya watu wenye hasira katika miji ya Nouakchott na Nouadhibou baadhi ya waandamanaji walidai kijana huyo auawe, wakidai kuwa Mohamed Ould Mohamed " alikufuru", na kumtuhumu kwamba alitoa maneno ya kishetani.

Kwa upande wake, Mohamed Ould Cheikh Mohamed alikanusha tuhuma dhidi yake, na kusema kuwa hakua na nia au lengo la kumuaibisha Mtume Muhammad, huku akibaini kwamba alihusishwa kwa nia ambayo hakua nayo. Katika makala aliyochapisha na kurusha kwenye mitandao tofauti, Mohamed Oul Mohamed alieleza kuwa uovu unaotendewa jamii ndogo wakati huu nchini Mauritania ulishuhudiwa katika karne ya kwanza ya Uislamu wakati wa Mtume Muhammad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.