Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Mauaji katika shule Nigeria: Boko Haram yanyooshewa kidole

Takribani wanafunzi 48 wameuawa na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu liliyotokea Jumatatu novemba 10 katika shule moja ya sekondari katika mji wa Potiskum kaskazini, mashariki mwa Nigeria.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan analaumiwa kwa kutowajibika kukomesha machafuko kaskazini mwa Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan analaumiwa kwa kutowajibika kukomesha machafuko kaskazini mwa Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mmoja kati ya waalimu, mlipuko wa bomu ulitokea kwenye saa moja na dakika 50 asubuhi saa za Nigeria (sawa na saa 12 na dakika 50 asubuhi saa za kimataifa) wakati wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana walikua katika mkutano wao wakila siku asubuhi, kabla ya kuanza visomo.

Miili ya wanafunzi waliouawa ilipelekwa hospitalini, huku wanafunzi zaidi ya 80, kwa mujibu wa Idara ya huduma za dharura, wakiwa wamejeruhiwa.
Hali hiyo ilizua hofu kwa wakaazi wa mji wa Potiskum. Msemaji wa Jeshi la Polisi la Nigeria, Emmanuel Ojukwu, amethibitisha tukio hilo, akisema "mlipuko uliosababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga" katika Chuo cha Potiskum.

Kulingana na mwalimu ambaye alinusurika shambulio hilo, mtu mmoja ambaye alijifananisha na wanafunzi ndiye aliye tekeleza shambulio hilo katikati ya mkutano wa wanafunzi. Hata hivyo mji wa Potiskum ulilengwa na shambulio la kujitoa mhanga wiki iliyo pita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya thelathini miongoni mwa watu kutoka jamii ya Washia walioshiriki katika sherehe za siku kuu ya Ashura.

Hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na shambulio hili liliyotokea Jumatatu Novemba 10. Tayari polisi imelituhumu kundi la Boko Haram, ambalo jina la kundi hilo linatafsiri “ marufuku kwa elimu ya mataifa ya magharibi”.

Jimbo la Yobe ni miongoni mwa majimbo ambayo yamekua yakilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayoendeshwa na kundi la Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amelani mauaji hayo akisema kwamba atafanya kiliyo chini ya uwezo wake ili wahusika wakamatwe na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo kiongozi huyo anatuhumiwa na baadhi ya raia kwamba hawajibiki kwa kukomesha machafuko katika maeneo yanayokabiliwa na mashambulizi mbalimbali.

Goodluck Jonathan anatazamiwa kutangaza Jumanne Novemba 11 kwamba atagombea katika uchaguzi wa rais ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.