Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: shambulio lawaua wanafunzi zaidi ya 45 Potiskum

Takribani wanafunzi 48 wameuawa na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu liliyotokea Jumatatu novemba 10 katika shule moja ya sekondari katika mji wa Potiskum kaskazini, mashariki mwa Nigeria.

Polisi imelituhumu kundi la Boko Haram kuhusika na shambulio liliyotokea Jumatatu Novemba 10 mwaka 2014 (kundi la Boko Haram kwenye mkanda uliyorushwa hewani Aprili 13 mwaka 2014).
Polisi imelituhumu kundi la Boko Haram kuhusika na shambulio liliyotokea Jumatatu Novemba 10 mwaka 2014 (kundi la Boko Haram kwenye mkanda uliyorushwa hewani Aprili 13 mwaka 2014). AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mmoja kati ya waalimu, mlipuko wa bomu ulitokea kwenye saa moja na dakika 50 asubuhi saa za Nigeria (sawa na saa 12 na dakika 50 asubuhi saa za kimataifa) wakati wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana walikua katika mkutano wao wakila siku asubuhi, kabla ya kuanza visomo.

Miili ya wanafunzi waliouawa ilipelekwa hospitalini, huku wanafunzi zaidi ya 80, kwa mujibu wa Idara ya huduma za dharura, wakiwa wamejeruhiwa.
Hali hiyo ilizua hofu kwa wakaazi wa mji wa Potiskum. Msemaji wa Jeshi la Polisi la Nigeria, Emmanuel Ojukwu, amethibitisha tukio hilo, akisema "mlipuko uliosababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga" katika Chuo cha Potiskum.

Kulingana na mwalimu ambaye alinusurika shambulio hilo, mtu mmoja ambaye alijifananisha na wanafunzi ndiye aliye tekeleza shambulio hilo katikati ya mkutano wa wanafunzi. Hata hivyo mji wa Potiskum ulilengwa na shambulio la kujitoa mhanga wiki iliyo pita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya thelathini miongoni mwa watu kutoka jamii ya Washia walioshiriki katika sherehe za siku kuu ya Ashura.

Hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na shambulio hili liliyotokea Jumatatu Novemba 10. Tayari polisi imelituhumu kundi la Boko Haram, ambalo jina la kundi hilo linatafsiri “ marufuku kwa elimu ya mataifa ya magharibi”.

Jimbo la Yobe ni miongoni mwa majimbo ambayo yamekua yakilengwa na mashambulizi ya mara kwa mara yanayoendeshwa na kundi la Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.