Pata taarifa kuu
UGANDA-Ushoga-Sheria

Sheria dhidi ya ushoga yafutwa nchini Uganda

Mahakama ya kikatiba nchini Uganda imefuta sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, iliyotiliwa saini na rais Yoweri Kaguta Museveni mwezi Februari mwaka huu,ikisema kuwa wabunge walioidhinisha sheria hiyo hawakutimiza idadi iliyokua inahitajika.

Mchungaji Martin Sempa (katikati) akiwa amezungukwa na wanaharakati wa kupambana na mashoga akiongea na waandishi wa habari baada ya Mahakama ya Katiba kufuta sheria ya kupambana na mashoga tarehe 1 Agosti 2014. AFP / ISAAC KASAMANI
Mchungaji Martin Sempa (katikati) akiwa amezungukwa na wanaharakati wa kupambana na mashoga akiongea na waandishi wa habari baada ya Mahakama ya Katiba kufuta sheria ya kupambana na mashoga tarehe 1 Agosti 2014. AFP / ISAAC KASAMANI AFP/ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Jaji Steven Kavuma aliiambia mahakama hapo jana kuwa Sheria hiyo ni "batili," kwa kuwa mchakato wake ulikiuka katiba, kwa kupita bila Kiwango stahili cha watunga sheria.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelezea uamuzi huo kama "ushindi kwa utawala wa sheria" na kutuma salamu za pongezi kwa wale wote waliochangia kufutwa kwa sheria hiyo hasa watetezi wa haki za binadamu nchini Uganda ambao hawakukaa kimya, na wakati mwingine wakijiweka katika hatari kubwa kutokana na suala hilo.

Sheria hiyo imekua imepiga marufuku mapenzi ya watu wa jinsia moja na kuwataka raia wa Uganda kuwafichua watu wote wanaojihusisha na vitendo vya ushoga ambapo waliobainika kujihusisha walikabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela, adhabu ambayo ililalamikiwa na jumuiya ya kimataifa.

Aidha wafadhili wengi wa Uganda ikiwemo Marekani  walifuta baadhi ya misaada waliyokua wakiitolea serikali ya nchi hiyo baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Mchungaji Martin Sempa, anaepinga ushoga, amesema Marekani itasababisha Uganda kukumbwa na laana kama ile ya Sodoma na Gomora, akilaani vikwazo viliyochukuliwa na Marekani dhidi ya Uganda kufuatia kupitisha sheria dhidi ya ushoga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.