Pata taarifa kuu
ICC-DRCONGO

Germain Katanga mbabe wa kivita katika jimbo la Ituri Mashariki mwa DRCongo akutikana na makosa ya uhalifu wa kivita

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC leo imetoa hukumu yake dhidi ya Germain Katanga, aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo kundi lake lilitekeleza mauji ya watu zaidi ya 2000 katika wilaya ya Ituri. Mahakama hiyo imemkuta na hatia ya makosa ya kivita, na kumsafisha kuhusu makosa ya ubakaji.

Germain Katanga, mbabe wa kivita katika eneo la Ituri
Germain Katanga, mbabe wa kivita katika eneo la Ituri
Matangazo ya kibiashara

Germain Katanga mwenye umri wa miaka 35 ametambuwa hatma yake hivi leo baada ya kufunguliwa mashtaka saba ya ukiukwaji wa haki za Binadamu, yakiwemo mauji na ubakaji wa wanawake wakati kundi lake la waasi la FRPI lilivamia raia wa Ituri mwaka 2003.

Mahakama hiyo ya ICC imesema Germain Katanga anahusika na mauaji ya Kivita na hana makosa ya ubakaji, na utumwa wa ngono.

Kesi ya Katanga imekuwa ikiendelea kwa miaka minne sasa tangu alipofikiswha Hague, na viongozi wa Mashaka amekuwa wakimtuhumu kuwa wakati wa uvamizi huo alikuwa na lengo la kuwamaliza kabisa watu wanaonshi katika kijiji cha Bogoro.

Jaji Bruno Cotte atasoma mchana huu hukumu mbele ya mahakama ya ICC dhidi Germain Katanga maharufu kama Lion ikiwa ni mara ya tatu mahakama hiyo kusoma hukumu dhidi ya mbabe huyo wa kivita anaye tuhumiwa makosa ya mauaji ya kivita, ubakaji.

Germain Katanga alikuwa kamanda wa kundi la FRPI, kundi ambalo wapiganaji wake wengi ni kutoka kabila la wa Lendu na Ngiti na ambao wanatuhumiwa kutekeleza mauaji ya kikabila dhidi ya watu wa kabila la wa Hema.

Mapigani ya kikabila kati ya makundi ya uasi yaliokuwa yakiwania ardhi ya Ituri yenye utajiri mkubwa wa rasilimali, huhusan dhahabu, mafuta na alimasi yalianza tangu mwaka 1999 na kugharimu maisha ya watu wanaokadiriwa kufikia elfu sitini.

Mbabe huyo wa zamani wa kivita anajitetea kutokuwa na hatia yoyote katika mauaji hayo, anatuhumiwa makosa ya mauaji ya kivita katika shambuli la Februari 24 mwaka 2003 katika kijiji cha Bogoro mjini Ituri

Katika kijiji hicho kulikuwepo na kambi ya kijeshi la watu wa kabila la wa Hema wa kundi la UPC la mbabe mwingine wa kivita Thomas Lubanga aliyehukumiwa na mahakama hiyo ya ICC mwaka 2012 kifungo cha miaka 14 jela kwa kosa la kuwaajiri watoto wadogo jeshini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.