Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRCongo

Jeshi la Burundi lakanusha uwepo wa kikosi chake katika ardhi ya DRCongo

Jeshi la Burundi limekanusha mwishoni mwa juma lililopita kuwepo kwa majeshi ya nchi hiyo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya madai ya Shirika la kitaifa la waandishi wa habari nchini Congo “Journaliste en danger” kulituhumu jeshi hilo kuendesha vitisho na vitimbi dhidi ya waandishi wa habari wawili wa tarafani Uvira katika mji wa Kiliba.

vijana wa chama tawala nchini Burundi wanaoshukiwa kupewa mafunzo katika ardhi ya DRCongo
vijana wa chama tawala nchini Burundi wanaoshukiwa kupewa mafunzo katika ardhi ya DRCongo Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Burundi Kanali Gaspard Baratuza ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa ikiwa waandishi wa habari wa DRC wanasumbuliwa na askari, basi askari hao watakuwa sio wa Burundi na kusisitiza kuwa hakuna hata askari mmoja wa Burundi katika ardhi y DRCongo.

Shirika la “Journaliste en danger” maarufu kama JED limetangaza kuwa Waandishi wa habari wawili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao ni wafanyakazi wa kituo cha redio katika jimbo la kivu ya Kusini tarafani Uvira mjini Kiliba eneo lijulikanlo Ondes na ambao wanafanya kazi katika kituo cha Radio Ondes FM wamelazimika kutoroka makwao kufuatia kusakamwa na askari wanaoshukiwa kuwa ni wa Burundi.

Hii inakuja baada ya waandishi hao wa habari kushirikiana na wenzano wa Burundi waliokwenda katika eneo hilo kufanya uchunguzi juu ya kuwepo kwa taarifa za vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD wanaopewa mafunzo na askari wa Burundi katika eneo hilo, taarifa ambayo ilikanushwa vikali na serikali ya Burundi.

Habari zaidi kutoka katika eneo hilo zinaarifu kuwa askari wa Burundi wanashuhudiwa katika bonde la Rusizi ambapo wanafuatilia harakati za kundi la waasi wa Burundi la FNL ambao wanashukiwa kupiga kambi katika eneo hilo, na hii ikiwa ni katika makubaliano ya siri kati ya burundi na DRCongo.

T

Pierre-Claver Mbonimpa, président de l'Aprodh au Burundi
Pierre-Claver Mbonimpa, président de l'Aprodh au Burundi martin ennals award / capture d'écran

aarifa hii ya uwepo wa wanajeshi wa Burundi katika ardhi ya DRCongo ambao wanatowa mafunzo kwa vijana wa chama tawala, ndio sababu ya kutiwa mbaroni kwa mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu na za wafungwa Pierre Claver Mbonimpa.

Hivi karibuni, chama kikuu cha upinzani cha Uprona chenye watu watu wengi kutoka jamii ya Watutsi kimejiondoa Serikalini hatuwa ambayo imeendelea kutia wasiwasi ya kutokea mgogoro wa kisiasa na hofu ya kuanza tena kwa mapigano ya kikabila wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka 2015 ambapo huenda Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi akawania tena muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.