Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Diplomasia

Jamhuri ya Afrika ya Kati : Operesheni Sangaris kuongezewa muda

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati imeomba jana operesheni Sangaris ya askari wa Ufaransa wa kulinda amani iongezewe muda nchini humo hadi mwaka 2015, baada ya uchaguzi mkuu. Akiwa ziarani mjini N'Djamena nchini Chad, rais wa mpito Catherine Samba-Panza amekiri kuwa serikali yake haina uwezo wa kuwahakikishia usalama wananchi wake waislamu ambao walikimbia nchini Chad na kuahidi kuwarejesha nyumbani wakati hali ya usalama itakuwa imeboreshwa.

Francisco Soriano, mkuu wa  kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa katika operesheni  Sangaris, februari 5 mwaka 2014 mjini Bangui.
Francisco Soriano, mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa katika operesheni Sangaris, februari 5 mwaka 2014 mjini Bangui. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

“Rais wa mpito (Catherine samba-Panza) ametueleza kwamba kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa wanatakiwa wasaliye hapa hadi uchaguzi, ikimansha mwanzoni mwa mwezi wa januari”, amesema rais wa halmashauri ya bunge ya Ufaransa, Elisabeth Guigou, ambae amekua akiongoza ujumbe wa wabunge tisa mjini Bangui, na baadae wamekutana kwa mazungumzo na rais Panza.

Kabla ya kutumwa kikosi hicho mjini Bangui mwanzoni mwa mwezi desemba, rais wa Ufaransa, François Hollande, alifahamisha kwamba operesheni ya kikosi hicho haitachukua muda mrefu, lakini jumamosi, waziri wa ulunzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, alisema operesheni hio “itachukua muda mrefu kama ilivyotarajiwa”.

Ijumaa, juma liliyopita, Paris ilichukua uamzi, kulingana na ombi la katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, kutuma wanajeshi 400 wa ziada, ambao watashirikiana na wanajeshi wengine 1600 wa Ufaransa na kufikia idadi ya wanajeshi 2000 wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Bunge la Ufaransa litachukua uamzi februari 25 kuhusu kuongezwa muda au la kwa kikosi cha Ufaransa kiliyo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuendelea na operesheni “Sangaris” ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa aprili.

Wakati huohuo, kaburi la watu wengi limegunduliwa jana mjini Bangui likiwa na miili ya watu kumi na tatu, baadhi yao wakiwa wamefungwa mikono, jambo ambalo linawauzunisha wengi na kumlazimu mwendesha mashitaka nchini humo bwana Ghislain Gresengue kuanzisha uchunguzi.

“Miili hiyo imepelekwa katika chumba maaluum cha hospitali cha kuhifadhia ili kuruhusu uchunguzi na kubaini lini matukio hayo yametokea, njia ambayo imetumika kutekeleza mauaji hayo, kwa kweli nalizungumzia nikiwa na uchungu moyoni pamoja na masikitiko makubwa, ila naamini kuwa wahusika watapatikana na kufunguliwa mashataka kwa mujibu wa Sheria”, amesema Gresengué Ghislain.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.