Pata taarifa kuu
SUDAN

Wafanyakazi wa Afya wa Umoja wa Mataifa wauawa jimboni Darfur

Wafanyakazi wawili wa afya raia wa Sudani wanaosaidia kutoa chanjo kwa watoto kwenye ukanda wa Darfur wameuawa, Umoja wa Mataifa umearifu leo Ijumaa na kulaani mauaji hayo. 

Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan  Ali Al- Za'tari
Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali Al- Za'tari unmultimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Marehemu hao, mtoa chanjo mmoja na dereva ,walikuwa sehemu ya timu inayotoa chanjo kwa watoto walio kwenye mazingira magumu dhidi ya maambukizi ya homa na vipele vyekundu kwenye ngozi huko Magharibi mwa Darfur imeeleza taarifa ya mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali Al-Za'tari.

Aidha Za'tari ametoa wito kwa pande zote kuhakikisha wanalinda wafanyakazi wote wanaotoa huduma na usaidizi kwa watu wengi wenye uhitaji kokote nchini Sudan.

Hata hivyo taarifa yake haikutoa maelezo zaidi kuhusu shambulio hilo lakini vyanzo vya Umoja wa Mataifa vimeiambia AFP kuwa tukio hilo linaonekana kuwa la kutekwa kwa gari siku ya Jumatatu.

Watu wenye silaha waliwaagiza wafanyakazi hao wa Afya kukabidhi gari lao na walipokataa , ndipo watu hao walipowaua kimesema chanzo hicho kwa masharti ya kutojulikana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.