Pata taarifa kuu
KENYA

Hatimaye wabunge nchini Kenya wakubali mshahara mpya

Wabunge nchini Kenya hatimaye wamekubali kulipwa mshahara waliokuwa wamependekezewa na Tume inayoshughulikia mishahara ya watumishi wa Umma nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Maafikiano hayo yalifikiwa baada ya mkutano ulioongozwa na Naibu rais William Ruto kati ya tume hiyo ya mishahara pamoja na ile ya bunge chini ya spika Justin Muturi.

Wabunge sasa watalazimika kupokea Shilingi za Kenya 532,500 kila mwezi kutoka Shilingi 800,000 walizokuwa wanataka kulipwa na hata wakati kutishia kusambaratisha shughuli za bunge.

Aidha, imeafikiwa kuwa wabunge hao watatozwa kodi na mshahara wao utaongezeka kila mwaka na mwisho wa miaka mitano mshahara wao utakuwa umefikia Shilingi Laki saba.

Pamoja na kukubali mshahara huo wabunge pia watalipwa posho za usafiri na kuhudhuria vikao vya bunge na pia watapewa mkopo wa kununua gari.

Miezi kadhaa sasa waandamanaji wamekuwa wakiandamana nje ya majengo ya bunge kupinga juhudi za wabunge kujiongezea mshahara na kukataa ule uliopendekezwa na tumehiyo.

Siku ya Jumanne waandamanaji hao walitumia damu ya ng'ombe na sanamu ya nguruwe kuonesha ulafi wa wabunge hao pamoja na pesa bandia wanayoita “Pesa Pig” kuwapa wabunge hao wakiingia kwenye vikao vya bunge.

Mwezi uliopita, maandamano mengine yalifanyika nje ya majengo ya bunge wakitumai nguruwe kuonesha gadhabu zao.

Awali, rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Raila Odinga kwa upande wao waliwataka wabunge hao kuachana na harakati zao za kutaka kulipwa mshahara mkubwa na badala yake kuwafanyia kazi wakenya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.