rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAF

Imechapishwa • Imehaririwa

Huenda Fatuma Samoura akapewa majukumu ndani ya CAF

media
Katibu Mkuu wa Fifa, Fatuma Samoura The Sun

Shirikisho la kandanda duniani FIFA na shirikisho la soka barani Afrika CAF zimefikia makubaliano ya kumteua Katibu Mkuu wa Fifa Fatuma Samoura kuwa mjumbe maalumu wa CAF katika uongozi wa soka.


Ikiwa uamuzi huo utaidhisnishwa Samoura ataanza rasmi kazi hiyo Agosti mosi na atahudumu kwa kipindi cha miezi sita.

Hatua hiyo inakuja katika kipindi ambacho CAF inakabiliwa na tuhuma za ukosefu wa maadili baada ya rais wa shirikisho hilo Ahmad Ahmad kuhojiwa na mamlaka za usalama nchini Ufaransa.

Vyanzo vya CAF vinasema ikiwa ataidhinishwa atalazimika kuachia baadhi ya majukumu yake ya kiutendaji katika Fifa.