Pata taarifa kuu
AFCON 2019-KENYA-SOKA-AFRIKA

Kikosi cha mwisho cha Kenya kuelekea AFCON nchini Misri, chatajwa

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Sébastian Migné  amekitaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kuelekea fainali ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Misri.

Kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne akiwaongoza wachezaji wa Harambee Stars kufanya mazoezi nchini Ufaransa Juni 11 2019
Kocha wa Harambee Stars Sebastien Migne akiwaongoza wachezaji wa Harambee Stars kufanya mazoezi nchini Ufaransa Juni 11 2019 footballkenya.org
Matangazo ya kibiashara

Michuano ya AFCON itaanza tarehe 21 mwezi Juni, na Kenya imepangwa katika kundi moja na Algeria, Senegal na Tanzania.

Kenya ambayo imerejea katika michuano hiyo baada ya miaka 15 itaanza kampeni yake dhidi ya Algeria tarehe 23 mwezi Juni.

Harambee Stars ipo nchini Ufaransa inakoendelea na maandalizi kuelekea katika michuano hiyo.

Kikosi kamili:

Makipa
Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo

Mabeki
Philemon Otieno, Abud Omar, Bernard Ochieng, Musa Mohammed, Joash Onyango, Joseph Okumu, David Owino, Eric Ouma

Viungo wa Kati
Victor Wanyama, Dennis Odhiambo, Erick Johanna, Ayub Timbe, Francis Kahata, Ismael Gonzalez, Ovella Ochieng, Paul Were, Johanna Omollo

Washambuliaji
Masud Juma, Michael Olunga, John Avire

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.