Pata taarifa kuu
KENYA-FIFA-SOKA

FIFA yachunguza ripoti ya kuepo kwa njama za kushindwa kwa Harambee Stars

Shirikisho la soka duniani FIFA, limethibitisha kuwa linachunguza ripoti ya kuwepo kwa matukio ya kupanga mechi ya timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, katika miaka iliyopita.

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya FIFA imekuja baada ya ripoti ya uchunguzi ya Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Nation, kuripoti kuwa beki wa zamani George Owino alihusika na kosa hilo kati ya mwaka 2009 mwezi Juni hadi mwezi Machi mwaka 2011.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo na wengine watatu ambao hawajatambuliwa walilipwa Mamilioni ya fedha za Kenya na rais wa Singapore, Raj Perumal ili kusababisha Harambee Stars kushindwa wakati wa michuano ya Kimataifa.

Kanuni za FIFA zinaeleza kuwa, mchezaji au yeyote anayebainika kuwa alihusika na kosa la upangaji wa matokeo, ataadhibiwa kwa faini ya Dola 100,000 na kufungiwa kutoshiriki katika masuala ya soka kwa angalau miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.