rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAF Michezo Afrika

Imechapishwa • Imehaririwa

Michuano ya kuwania taji la Shirikisho baina ya vlabu barani Afrika yaendelea

media
Kikosi cha wachezaji wa AS Vita Club. AFP PHOTO / JUNIOR D.KANNAH

USM Alger ya Algeria, AS Vita Club ya DRC, ASEC Mimosas ya Cote d'Ivoire, na Al Masry ya Misri, tayari zimefuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho baina ya vlabu barani Afrika mwaka huu.


Hii ni kufuatia ushindi wa mzunguko wa pili wa michuano ya mwondoano siku ya Jumanne usiku.

USM Alger ilishinda Plateua United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 5-2, baada ya ushindi mkubwa wa mabao 4-0 hapo siku ya Jumanne wiki hii wakiwa nyumbani.

AS Vita Club nao wakicheza ugenini waliwafunga CS La Mancha ya nchi jirani ya Congo Brazaville mabao 5-1 na hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 6-1.

Michuano hiyo inaendelea Jumatano wiki hii kupata timu nyingine 12 zitakazofuzu katika hatua hiyo ya makundi kabla ya kufanyika kwa hatua ya droo tarehe 21.

Ratiba ya leo:

Welayta Dicha vs Young Africans

CARA Brazaville vs Saint George

Akwa United vs Al Hilal Omdurman

SuperSport United vs Gor Mahia

Costa do Sol vs Rayon Sport

Raja Casablanca vs Zanaco.