Pata taarifa kuu
RIADHA

Jiji la Kampala kuandaa mashindano ya riadha ya nyika ya dunia siku ya Jumapili

Mashindano ya riadha ya nyika ya dunia yatafanyika siku ya Jumapili jijini Kampala nchini Uganda wakati huu wanariadha mbalimbali wakianza kuwasili katika jiji hilo.

Wanariadha wakishiriki katika mashindano yaliyopita ya Nyika
Wanariadha wakishiriki katika mashindano yaliyopita ya Nyika pbs
Matangazo ya kibiashara

Wanariadha zaidi ya 500 watashiriki katika mbio hizo kutoka mataifa 59.

Makala haya ya 41, kwa mara ya kwanza yanawajumuisha wanariadha wa Sudan Kusini ambao kwa sasa ni wakimbizi.

Wanariadha hao watapambana katika mbio za Kilomita 10 kwa wanaume na wanawake.

Mbali na mbio hizo wanariadha chipukizi watashindana katika mbio za Kilomita 8 kwa upande wa wanaume huku wanawake chipukizi wakikimbia katika mbio za Kilomita 6.

Mataifa mengine ya Afrika ambayo yamewahi kuwa wenyeji wa mashindano haya ni pamoja na Morocco mara mbili mwaka 1975 na 1998.

Afrika Kusini mwaka 1996 na Kenya mwaka 20017.

Makala ya 40 ya mashindano haya yalifanyika mwaka 2015 jijini Guiyang nchini China.

Mabingwa wa mwaka 2015:-
Kilomita 12 kwa upande wa wanaume- Geoffrey Kipsang kutoka Kenya.

Kilomita 8 kwa wanariadha chipukizi kwa upande wanaume- Yasin Haji kutoka Ethiopia.

Kilomita 8 kwa upande wa wanawake-Agnes Jebet Tirop kutoka nchini Kenya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.