Pata taarifa kuu
URUGUAY-ITALIA-Sheria-Michezo

Luis Suarez apunguziwa adhabu

Mahakama inayoshughulikia makosa ya michezo imekubaliana na hukumu ya kusimamishwa kwa muda wa miezi minne iliyotolewa na shirikisho la soka dunia FIFA dhidi ya Luis Suarez, raia wa Uruguay.

Mchezaji wa kimataifa, raia wa Uruguay, Luis Suarez alifungiwa kushiriki mechi yoyote kwa muda wa miezi minne baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini, wakati wa mechi ya kombe la dunia 2014 kati ya Uruguay na Italia.
Mchezaji wa kimataifa, raia wa Uruguay, Luis Suarez alifungiwa kushiriki mechi yoyote kwa muda wa miezi minne baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini, wakati wa mechi ya kombe la dunia 2014 kati ya Uruguay na Italia. REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Lakini mahakama hiyo imefuta adhabu nyingine iliyochukuliwa na shirikisho hilo dhidi ya mchezaji huyo ya kushiriki mazoezi na kabu yake mpya ya Barcelona.

Majaji wa mahakama hiyo ya Lausanne nchini Uswisi wamebaini kwamba hukumu iliyochukuliwa na FIFA dhidi ya Luis Suarez baada ya kumng'ata beki wa Italia ina endana na kosa alilofanya, lakini adhabu ya kumsimamisha kufanya mazoezi haikua sahihi, wamesema majaji hao.

Awali mashabiki wa Suarez walikua na imani kwamba huenda mahakama hiyo ikachukua uamzi wa kupunguza hukumu iliyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA la kumsimamisha kucheza kwa muda wa miezi minne, baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini, katika michuano ya kombe la dunia, wakati timu yake ya Uruguay ilikua ikicheza na timu ya taifa ya Italia kwenye Uwanja wa Natal.

Agosti 8 mwaka 2014, mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uruguay alijaribu kujitetea mbele ya majaji watatu wa mahakama inayoshughulikia makosa ya michezo TAS katika mji wa Lausanne, nchini Uswisi, na uamzi unasubiriwa kutolewa jumatano saa tisa saa za kimataifa (sawa na saa saba saa za Afrika ya Kati, ikiwa sawa na saa nane saa za Afrika Mashariki).

Mwezi Julai, Luis Suarez alinunuliwa na klabu ya Barcelona akitokea katika klabu ya Liverpool, lakini tangu hukumu dhidi yake ichukuliwe, Luis Suarez hajarudi uwanjani kushiriki mazoezi na wenzake wa klabu ya Barcelona. Alichukuliwa hukumu ya kufungiwa mechi kwa muda wa miezi tisa bila kuichezeya timu yake ya Uruguay katika michuano ya kombe la dunia, na kusimamishwa kwa muda wa miezi minne katika shughuli zote za soka.

Rais wa shirikisho la soka duniani, Joseph Blatter alitaja kuwa hukumu hiyo ni kali mno.

Chama cha wachezaji FIFPRO, kilitolea wito mahakama inayoshughulikia makosa ya michezo TAS kuhusu hukumu hiyo, kikibaini kwamba inakiuka haki za Suarez.

Lakini FIFA ilichukua hukumu hiyo kutokana na mchezaji mwenyewe, ambaye alijihusisha mara kadhaa na tabia yake hiyo ya kung'ata wachezaji wenziye katika michuano mbalimbali.

Mara ya kwanza, Luis Suarez alimng'ata mchezaji mwenziye alipokua akiichezea klabu ya Ajax Amsterdam, akarudi kosa hilo alipokua akiichezea Liverpool, katika mechi yake na Chelsea, na kwa mara ya tatu katika mchezo wa michuano ya kombe la dunia kati ya timu yake ya Uruguay na Italia mwezi Juni mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.