Pata taarifa kuu
VENEZUELA-UPINZANI-HAKI

Wapinzani Venezuela kufunguliwa mashtaka

Nchini Venezuela Bunge jipya la Katiba limepiga kura kwa kauli moja ya upinzani kushtakiwa kwa makosa ya uhaini, baada ya kushtumiwa kuomba Marekani kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro awashtumu viongozi wa upinzani kuwa upande wa Marekani.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro awashtumu viongozi wa upinzani kuwa upande wa Marekani. REUTERS/Marco Bello
Matangazo ya kibiashara

Rais Nicolas Maduro amekuwa akiwashtumu viongozi wa upinzani kuwa upande wa Marekani, nchi ambayo amesema inalengo la kuivamia kijeshi nchi yake.

Wiki iliyopita Rais Donald Trump aliamuru vikwazo vipya kwa Venezuela.

Washington tayari tangu kabla ya uchaguzi huo ilimuwekea vikwazo vya kisheria na kifedha Rais Maduro, na kumwita "dikteta".

Agosti 10 mwaka huu, Marekani ilichukua hatua mpya dhidi maafisa wanane wa serikali ya Venezuela, ikiwa ni pamoja na kaka wa aliyekua rais wa nchi hiyo Hugo Chavez. Hugo Chavez alitawala nchi hiyo toka 1999 hadi 2013.

Mabaraza mawili ya Bunge hatimaye yanagongana nchini Venezuela, huku yakiendesha shughuli zao katika jengo moja la serikali. marekani tayari imeonyesha msimamo wake. Hivi karibuni Waziri wa Fedha wa Marekani alielezea utayari wa nchi yake ya kuunga mkono upinzani ambao unapambana dhidi ya dhulma," na kwa sasa, Marekani imechukua vikwazo vinavyowalenga maafisa wanane wa serikali ya Venezuela, kwa minajili ya kusalimu amri.

Majina mapya manane yamewekwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Marekani na kupiga marufuku wananchi wa Marekani kuendesha shughuli za kibiashara na maafisa hao. Miongoni mwao, mi nduguye Hugo Chavez, shujaa wa Mapinduzi ya miaka 2000, ambapo Rais Nicolas Maduro ni mrithi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.