Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Idadi ya watu waliokufa katika shambulio la Bomu Somalia yafikia 276

Watu 276 wamethibitishwa kufa na wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa baada ya shambulio baya zaidi la bomu la kutegwa kwenye lori kuwahi kutekelezwa mjini Mogadishu nchini Somalia. 

Mwanamke wa Somalia akiomboleza kwenye eneo la mlipuko mtaa wa KM4 mjini Mogadishu. Tarahe 15 Octoba 2017
Mwanamke wa Somalia akiomboleza kwenye eneo la mlipuko mtaa wa KM4 mjini Mogadishu. Tarahe 15 Octoba 2017 REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa jiji la Somalia wameendelea kujitokeza kutafuta ndugu zao waliopotea baada ya shambulio hili la siku ya Jumamosi, shambulio ambalo liliharibu pia majengo kadhaa yaliyokuwa jirani.

Serikali ya Mogadishu inasema kuwa kwa sasa operesheni maalumu inaendelea na kwamba majeruhi kadhaa bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali mjini Mogadishu.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, siku mbili baada ya nchi yake kukumbwa na mauaji mabaya kabisa kuwahi kutokea tangu mwa mwaka 2007.

Takriban watu 230 waliuawa siku ya Jumamosi kwenye milipuko Mogadishu. Mamia ya watu wengine wanaripotiwa kujeruhiwa.

Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.

Lakini mpaka sasa hakuna kundi hata moja ambalo limejitokeza na kudai kuhusuka na mauaji hayo yaliyotokea kwenye eneo linalotembelewa na watu wengi katikati mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Shambulio hili lilitokea saa chache baada ya Waziri wa Usalama wa raia nchini humo na Mkuu wa majeshi kujuzulu kwenye nafasi zao.

Katika shambulio la kwanza, bomu lilokuwa kwenye lori, lililipuka kwenye njia panda, iitwayo Kilomita-5, ambapo kuna ofisi za serikali, mahoteli na maduka, vyote viliporomoka katika mlipuko huo.

Saa mbili baadaye, bomu jengine lilikalipuka katika mtaa wa Medina.

Mlipuko huo ulitokea dakika chache tu baada ya lori lililoegeshwa na vilipuzi kulipuliwa karibu na

Baadhi ya mashahidi wanasema kuwa hoteli ya Safari ilianguka huku watu kadhaa wakidaiwa kukwama chini ya vifusi vyake, wakiongeza kuwa wanaamni kuwa watu wengi waliangamia katika mlipuko huo.

lango kuu la hoteli, kwa mujibu wa polisi.

Mashambulizi mengi ya kundi la Al Shabab yamekua yakiulenga mji wa Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.