Pata taarifa kuu
KENYA-UNHCR-Haki za binadamu

UNHCR yainyoshea Kenya kidole cha lawama

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi nchini Kenya UNHCR, limeelezwa kuguswa na kushtushwa na taarifa za kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji vinavyodaiwa kufanywa na polisi wa nchi hiyo dhidi ya raia wa Kisomali.

Wakimbizi wa Somalia wakikamatwa mjini Nairobi nchini Kenya.
Wakimbizi wa Somalia wakikamatwa mjini Nairobi nchini Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

UNHCR inasema kuwa imepokea taarifa kuhusu kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa raia wa Somalia wanaokamatwa na maofisa usalama wa Kenya ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwenye jela zilizojaa huku mazingira ya kibinadamu yakiwa hayaruhusu.

Shirika hilo limeongeza kuwa linahofu kuhusu operesheni inayoendelea dhidi ya ugaidi nchini humo kuwalenga raia wa Somalia peke yake, kitendo ambacho sasa kimepelekea wengi wa raia hao kuishi wa wasiwasi.

Alex Mbilinyin naibu mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya, amesema licha ya kushuhudia kurejeshwa nyumbani kwa raia wa Somalia waliokuwa wanashikiliwa kwenye uwanja wa Ksarani, bado zoezi hili lina changamoto.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu pamoja na wataalam katika masuala ya haki za binadamu walilani zoezi hili.

Zoezi hili la msako na kushikiliwa kwa idadi kubwa ya raia wa Somalia, kwa mujibu wa viongozi wa Kenya, ni kukabiliana na ugaidi na uhamiaji haramu, kunaweza kusababisha kuongezeka kwa visa vya ubaguzi”, amebaini Cedric Barnes, afisa wa Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Migogoro ICG (ICG).

“Hali hii itapelekea wanamgambo wa kislamu wa kundi la al Shabab wanakua na nguvuna kuzidisha mashambulizi”, amesema Barnes.

Kundi hilo la wanamgambo wa kislamu la al Shabab kutoka Somalia lilikiri kuhusika katika shambulio dhidi ya jumba la kibiashara la Westgate, ambalolilisababisha vifo vya watu 67.

Raia wa Somalia waliyofukuzwa nchini Kenya wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mogadiscio, aprili 9 mwaka 2014.
Raia wa Somalia waliyofukuzwa nchini Kenya wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mogadiscio, aprili 9 mwaka 2014. REUTERS/Feisal Omar

Juma liliopita, shirika la kimataifa linalotetea hki za binadamu, lilituhumu serikali ya Kenya kutumia raia wa Somalia katika vitendo vya kuwakejeli, na baadae kuwanyanya, shirika hilo likibaini kwamba liliwaona askari polisi wakiwapiga na kuwatukana wafungwa, huku askari polisi hao wakiwaibia hela zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.