Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Kesi ya washukiwa 4 wa ugaidi kwenye jumba la Westgate yaahirishwa hadi mwakani: RFI

Mahakama kuu jijini Nairobi nchini Kenya imeahirisha kesi inayowakabili watuhumiwa wanne raia wa Somalia kwa kuhusika kwao kwenye shambulio la kigaidi la Westgate mwezi mmoja uliopita.

Mmoja wa watuhumiwa waliotekeleza shambulio kwenye jumba la Westgate akionekana kwenye picha za CCTV
Mmoja wa watuhumiwa waliotekeleza shambulio kwenye jumba la Westgate akionekana kwenye picha za CCTV Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa wanne wa kupanga njama za shambulio la Westgate walipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Milimani kusomewa mashtaka yanayowakabili ambapo kesi yao iliahirishwa hadi tarehe 15 mwezi January mwakani.

Majaji wanaosikiliza kesi hiyo wamesema kuwa kesi yao itaanza kusikilizwa rasmi mwakani mwezi January wakati huu ambapo maofisa usalama wakiendelea kukusanya ushahidi kuwahusisha na tukio hilo

Mahakama imeongeza kuwa watuhumiwa hao wanne watajua hatma yao hapo mwakani iwapo watapatiwa dhamana au la kulinga na makosa ambayo yako mbele yao ya kuhusika na kuwasaidia watu waliotekeleza shambulio la Westgate.

Watuhumiwa hao raia wa Somalia ni pamoja na Liban Abdulah, Hussein Hassan na Adan Mohamed ambao wote kwa pamoja hawakutakiwa kujibu chochote.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu James Shimanyula aliyekuwepo mahakamani upande wa mashtaka ulita watuhumiwa hao wasipatiwe dhaman kutokana na makosa yanayowakabili kuwa ni yaugaidi yasiyohitaji dhamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.