rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Muziki

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwimbaji wa mitindo ya Rock Tom Petty amefariki dunia

media
Mimbaji nguli Tom Petty. Twitter Tom Petty

Mwimbaji mashuhuri kutoka Marekani Tom Petty ambaye alikua akiimba kwa kutumia gita amefariki, kwa mujibu wa familia yake.


Alifariki siku ya Jumatatu usiku, Oktoba 2 kutokana na maradhi ya moyo.

"Tunasikitika na kifo cha baba yetu, mume, ndugu, kiongozi na rafiki Tom Petty," familia ya mwanamuziki huyo imesema.

Tom Petty amefariki akiwa na umri wa miaka 66.

Awali vyombo vya habari vya Marekani vilisema kwamba Tom Petty yupo mahututi hospitalini akisumbuliwa na shambulizi la moyo.

Mwimbaji huyo alikutwa nyumbani kwake siku ya Jumapili akiwa ameanguka chini na hajitambui, na baadae kukimbizwa hospitalini.

Anafahamika kwa nyimbo nyingi ikiwemo 'American Girl' na 'I won't back down'.