rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Muigizaji wa Marekani Jerry Lewis afariki dunia akiwa na umri wa miaka 91

media
Jerry Lewis katika tamasha la 66 la Cannes akicheza filamu ijulikanayo kama "Max Rose", Mei 23, 2013.. REUTERS/Regis Duvignau

Muigizaji mkuu wa Marekani Jerry Lewis, mfalme wa vichekesho nchini humo, alifariki dunia siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 91 nyumbani kwake katika jimbo la Las Vegas, familia yake imesema.


Alizaliwa mwaka 1926 katika mji wa Newark, katika jimbo la New Jersey, na alipata mafanikio makubwa katika kazi yake ya kila siku hasa katika filamu kama Mpenda wanawake (mwaka 1961) au Doctor Jerry and Mister Love (mwaka 1963), baada ya kushirikiana mwanzoni na mwimbaji Dean Martin.

Jerry Lewis "mcheshi maarufu, muigizaji na mtunzi mkuu wa hadithiamefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 91 nyumbani kwake katika jimbo la Las Vegas, akiwa pamoja na familia yake," ndugu zake wamesema katika taarifa yao.

Msemaji wake, Candi Cazau, amesema kwa simu kwamba kifo chake kililitokea saa 3:30 asubuhi (sawa na saa 10:30 saa za kimataifa).

Jerry Lewis alielezea kazi yake kwa maneno haya: "Nilifanikiwa sana nikiwa mjinga kabisa." "Niliangalia ulimwengu kwa macho ya mtoto tangu nilipokuwa na umri wa miaka tisa," alisema katika mahojiano na shirika la habari la Reuters mwaka 2002. "Nilibaki hivo. Nilifanya kazi. nzuri, " Jerry Lewis aliongeza

Alijulikana sana Ulaya na hasa nchini Ufaransa.Alipewa tuzo ya heshima mwaka 1984 na Jack Lang, wakati huo Waziri wa Utamaduni.