Pata taarifa kuu
CANNES 2017-TAMASHA

Tamasha la Cannes 2017 laendelea kwa siku ya tisa ya mashindano

Tamasha la filamu la Cannes 2017 limeingia leo siku yake ya tisa ambapo wasani mbalimbali wanaendelea kupambana.Tayari kizazi kipya cha New York cha filamu za kujitegemea kimejikusanyia umaarufu katika tamasha hili ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki, huku nyota ya msani Nicole Kidman ikionekana kufifia.

Wasani nyota mbalimbali wanashiriki tamasha la kimataifa la 70 linaloendelea kusini mwa Ufaransa.
Wasani nyota mbalimbali wanashiriki tamasha la kimataifa la 70 linaloendelea kusini mwa Ufaransa. REUTERS/Regis Duvignau
Matangazo ya kibiashara

Katika tamasha hili la kimataifa la 70ambalo linaendelea kusini mwa Ufaransa hadi Jumapili, wasani mbalimbali wanaendelea kushiriki katika mashindano mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Golden Palm, yale ya wanamuziki na mengineo. Filamu kadhaa zinazozungumzia kuhusu ukweli wa Afrika, katika sehemu sambamba zimeendelea kupiga fora katika tamasha hili la kimataifa. Filamu inayopewa jina la "Makala" ya raia kutoka Ufaransa Emmanuel Gras, iliyotengenezwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilionyeshwa Jumatano katika wiki ya ukosoaji '.

Nchini DRC, kijana mmoja mwanakijiji  anatarajia kua na maisha bora ya baadaye kwa ajili ya familia yake, akielekea katika maeneo mbalimbali kuuza matunda ya kazi yake.
Nchini DRC, kijana mmoja mwanakijiji anatarajia kua na maisha bora ya baadaye kwa ajili ya familia yake, akielekea katika maeneo mbalimbali kuuza matunda ya kazi yake. Photo: Bathysphère production.

Makala inamaanisha "makaa ya mawe" kwa Kiswahili. Makaa haya ya mawe yanatemgenezwa na mkulima mdogo wa jimbo la Katanga Kabwita Kasongo. Emmanuel Gras aliweza kumnasa akikata mti akitumia shoka, kisha aichukua mti huo akaukata vipande vodogo vidogo (kuni), kabla ya kujenga tanuri kwa minajili ya kuchoma kuni. Kisha anaweka bidhaa hiyo ambayo aliweza kuchoma kwenye mifuko mizito na kuiweka kwenye baiskeli. Kisha anasafiri na makaa hayo hadi kilomita zaidi ya hamsini kwa na kuiuza katika mji wa Kolwezi.

Kabwita Kasongo, mwenye umri wa miaka 28, baba wa watoto watatu ana matumaini ya kupata fedha za kutosha kwa kukidhi maisha bora ya baadaye kwa ajili ya familia yake. Pamoja na juhudi za Kabwita Kasongo, tayari mtu anaona hadithi za kale, kama ile ya Sisyphus katika zama za Kigiriki aliyehukumiwa kusukuma milele hadi juu ya kilima mwamba ulioshuka mara moja juu.

"Kutengenezwa kwa filamu hii"

"Filamu hii ilitengenezwa kwa picha, baada ya kuona watu wakisukuma baiskeli hizo, kwa kweli niliona kitu kimoja cha ajabu sana, anasema Emmanuel Gras. Na nkupiti picha hii, niliona kuwa watu wengi walipitia maisha haya ili kufikia maisha mazuri. Hadithi hupelekea mtu kuwaza mbali na kufanya mambo mazuri, " ameongeza Bw Gras

Emmanuel Gras alimaliza kutengeneza filamu hiyo siku chache kabla ya kuionyesha katika tamasha la kimataifa la Cannes. Ana matumaini ya kurudi Katanga kabla ya mwaka mmoja ili kumuonyesha Kabwita Makala Kasongo na kijiji chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.