Pata taarifa kuu
FILAMU-MUZIKI-TAMTHILIA

Emma Stone na Casey Affleck waibuka washindi wa Tuzo za Oscar

Emma Stone na Casey Affleck ambao wametajwa kuwa waigizaji bora wametunukiwa tuzo za oscar mwaka huu. Tuzo kuu imekwenda kwa Picha bora ya mwaka , filamu ya muziki ya La La Land imetajwa kuwa filamu bora mwaka huu.

Emma Stone na Ryan Gosling katika filamu iiwayo « La La Land », ya Damien Chazelle.
Emma Stone na Ryan Gosling katika filamu iiwayo « La La Land », ya Damien Chazelle. SND
Matangazo ya kibiashara

"Moonlight" inaelezea hadithi ya Chiron, kijana kutoka moja ya vitongoji vya mji wa Miami, nchini Marekani ambaye amekua akijaribu kupata nafasi yake katika ulimwengu huu. Emma Stone ametunukiwa tuzo hiyo kwa nafasi yake katika filamu bora ijulikanayo kwa jina la "La La Land" na Casey Affleck kwa kazi nzuri aliyoifanya katika filamu iitwayo "Manchester by the sea."

Wakati huo huo, mwigizaji nyota Denzel Washington ametajwa kuwa mtunzi bora katika filamu hiyo.

Denzel Washington , ni miongoni mwa nyota wa kiafrika waliokua wakigombea kushinda tuzo yenye umbo la sanamu ya dhahabu baada ya kutowakilishwa kwa miaka miwili, jambo ambalo liliibua kampeni iliyopewa jina la Oscar ni ya watu weupe.

Timu iliyocheza filamu iitwayo «La La Land» katikati akiwemo Emma Stone na Ryan Gosling.
Timu iliyocheza filamu iitwayo «La La Land» katikati akiwemo Emma Stone na Ryan Gosling. NBC/Reuters

Maandalizi ya mwaka huu yamekuwa magumu kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo maandamano, na hali mbaya ya hewa ambayo haikutarajiwa iliyopiga eneo la California.

Zulia jekundu lilitandikwa katika ukumbi wa Dolby uliopo jijini Los Angeles kwa ajili ya sherehe za mwaka huu za Oscars.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.