Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Brussels na London watofautiana kuhusu mazungumzo yajayo

Tume ya Umoja wa Ulaya imepitisha Jumatatu asubuhi wiki hii maswala muhimu ya mazungumzo ambayo inatarajia kufanya na Uingereza kwa mkataba wa baadaye baada ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Desemba 31, 2020.

Boris Johnson wakati wa hotuba yake kuhusu hatma ya Uingereza baada ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya huko London, Februari 3, 2020.
Boris Johnson wakati wa hotuba yake kuhusu hatma ya Uingereza baada ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya huko London, Februari 3, 2020. Frank Augstein/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, kwa upande mwingine katika kipindi chote hicho, Waziri Mkuu wa Uingereza pia amewasilisha maono yake.

Katika mazungumzo yanayokuja, Tume ya Umoja wa Ulaya inapendekeza masuala matatu muhimu, mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet, amebaini.

Swala la kwanza, na muhimu zaidi, ni lile la mkataba wa kibiashara. Pamoja na maswala mengine nyeti: jinsi ya kuhakikisha kuwa bidhaa na na biashara vinaweza kubadilishwa, jinsi ya kuhakikisha soko la huduma, jinsi ya kumaliza maswali ya forodha ... Yote haya kwa kuweka dhamana ya kufuata sheria kwa pande zote ili kuepuka hali za ushindani usio sawa.

Maswala mengine mawili ya mazungumzo pia yamewasilishwa: swala la ushirikiano wa ulinzi na usalama, ushirikiano wa polisi na mahakama na sehemu inayojulikana ya utawala, ili kupanga jinsi ya kuchunguza kwa karibu uheshimishwaji mzuri wa mikataba ijayo.

Kwa upande wa Michel Barnier, ambaye atasimamia mazungumzo haya, amesema muda wa mazungumzo ni mfupi sana na hata ikiwa mazungumzo yatakuwa na malengo muhimu, hakuna imani kwamba hadi Desemba 31 kuna hatua yoyote itakuwa imepigwa.

Hayo yanajiri wakati Waziri Mkuu wa Uingereza Borsi Johnson leo anatarajiwa kuainisha masharti ya nchi yake kuelekea mazungumzo ya ushirikiano wa siku za usoni na Umoja wa Ulaya baada ya Uingereza kukamilisha mchakato wa Brexit. Duru kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyopo mtaa Downing zinasema Johnson atatumia hotuba yake ya leo kusisitiza kuwa Uingereza itastawi baada ya Brexit hata kama haitofanikiwa kufikia makubaliano ya kibiashara na Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.