Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Brexit: Mchakato wa Uingereza kujitoa EU kukamilika Februari 1

Muda wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya utakamilika usiku wa manane Ijumaa, sawa na siku 1,317 baada ya uamuzi wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. Wengi wanajiuliza kitakacho badilika Februari 1.

Mmoja wa waandamanaji wanaopinga Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya akishikilia bendera ya umoja huo mbele ya makao makuu ya Bunge, London, Oktoba 25, 2019.
Mmoja wa waandamanaji wanaopinga Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya akishikilia bendera ya umoja huo mbele ya makao makuu ya Bunge, London, Oktoba 25, 2019. REUTERS/Henry Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Biashara na shughuli mbalimbali za kila siku kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya zitaendelea kama hapo awali hadi mwisho wa mwaka 2020.

Katika kipindi hiki cha mpito cha miezi 11, London na Brussels watajadili uhusiano wao wa baadaye. Hata hivyo mabadiliko kadhaa yatakuwa yanafanyika.

Ijumaa saa sita usiku, Umoja wa Ulaya kwa mara ya kwanza utapoteza nchi mshirika, ambayo ni moja wapo ya nchi kubwa na tajiri zaidi katika umoja huo.

Kujiondoka kwa Uingereza yenye wakazi milioni 66 katika Umoja wa Ulaya (EU), umoja huo utajikuta idadi ya raia wake inapunguka hadi milioni 446. Ardhi yake itapungua kwa 5.5%.

Ikiwa Uingereza itaamua kurudi, italazimika kupitia utaratibu wa kawaida wa uanachama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.