Pata taarifa kuu

Mauaji ya G. DUPONT na C. VERLON: Seneta Sueur amtaka Waziri wa Majeshi kutoa mwanga zaidi

Seneta mmoja wa Ufaransa kutoka chama cha Kisocialisti Jean-Pierre Sueur ametoa wito kwa Waziri wa Majeshi nchini Ufaransa Florence Parly kuhusu giza lililopo katika kesi ya mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon, waandishi wa habari wawili wa RFI waliuawa huko Kidal nchini Mali Novemba 2, mwaka 2013.

Seneta Jean-Pierre Sueur katika kikao cha Baraza la Seneti, Januari 14, 2020.
Seneta Jean-Pierre Sueur katika kikao cha Baraza la Seneti, Januari 14, 2020. © Sénat
Matangazo ya kibiashara

Swali lake limekuwa linahusiana na vidokezo kadhaa maalum hususan hadhi ya mmoja wa wateka nyara, ambaye alikuwa akiwasiliana na idara za ujasusi za Ufaransa miezi kadhaa kabla ya kutokea kwa mauaji hayo, na muingiliano wa kuachiwa kwa mateka wa Arlit pamoja na utekaji nyara wa wandishi hao wawili pamoja na jukumu la vikosi maalum vya Ufaransa katika utafutaji wa mateka.

Janga hilo, kiungo kinachowezekana kati ya kutolewa kwa mateka wa Arlit na utekaji nyara wa waandishi wa habari hao wawili na mwishowe jukumu la vikosi maalum vya Ufaransa wakati wa utafutaji na vile vile asili ya harakati iliyozinduliwa.

Seneta Jean Pierre Sueur amesema hajaridhishwa na majibu yanayotolewa.

“Ninasikitika kwa sababu katika tukio lenye hali ya umma, ambayo imewekwa wazi na uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari na kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, serikali inapaswa kusema lolote na kueleza ikiwa ni ukweli au uwongo, Kwa familia, jamaa, marafiki na wenzake wa waandishi hawa wawili waliouawa, hakuna kitu kibaya zaidi kama ukimya” , Seneta Jean Pierre Sueur amesema.

Claude Verlon na Ghislaine Dupont waliuawa huko kaskazini mwa Mali siku kadhaa baada ya kutekwa nyara ambapo uchunguzi kuhusu mazingira ya kutekwa hadi kuuawa kwao mpaka sasa bado hujawekwa bayana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.