Pata taarifa kuu
MAREKANI-UFARANSA-NATO-USALAMA

Trump amshambulia Macron kwa kukejeli NATO

Rais wa Donald Trump amemshambulia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 70 ya NATO na kutusi mkutano ulioandaliwa katika hali tete kati ya wanachama wa jumuiya hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump amemshambulia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 70 ya NATO.
Rais wa Marekani Donald Trump amemshambulia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 70 ya NATO. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho haya hayakuwa na sherehe kubwa kutokana na kuibuka tofauti kati ya wanachama kuhusu Syria au ufadhili wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi (NATO), huku Emmanuel Macron akizusha sintofahamu baada ya kusema kuwa NATO ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1949 ni 'ubongo uliokufa'.

Mkutano huo unaotajarajiwa kuanza hii leo Jumanne, tayari umekumbwa na mzozo mkali kati ya wanachama wake, hususan Ufaransa na Uturuki, pamoja na muendelezo wa suala la mchango wa mataifa mwanachama.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema kwamba atapinga mpango wa Nato wa kiulinzi kwa nchi za Baltiki iwapo haitaiunga mkono Uturuki katika vita vyake dhidi ya kikundi cha Kikurdi ambacho inakichukulia kama kigaidi.

Hata kabla ya vikao rasmi Jumanne usiku katika eneo la Buckingham na Jumatano kwenye uwanja wa gofu wa kifahari nje kidogo ya mji wa London, Rais wa Donald Trump amemkosoa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kusema Nato ni 'ubongo uliokufa'.

Huu ni 'uamuzi mbaya sana tena sana kwa nchi 28,' Donald trump ameongezea katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg. Donald Trump amesema 'ameshangazwa sana' na kauli ya Emmanuel Macron, ambaye anatarajia kukutana naye kwa mazungumzo leo Jumanne, huku akibaini kwamba kauli hiyo 'ni hatari sana' kwa Ufaransa.

"Kwa wakati huu hakuna anayehitaji usaidizi wa Nato kama Ufaransa... Manufaa inayopata Marekani ni machache mno. Huu ni usemi hatari sana. "Ninamwangalia [Bwana Macron] kisha najiambia, anahitaji ulinzi zaidi ya mwengine yoyote hivi sasa lakini pia namuona akijiondoa kutoka kwa Nato. Hata hivyo ni jambo ambalo halijanishangaza kwa kweli."

Bwana Macron alielezea muungano huo kama "ubongo uliokufa", akisisitiza kile anachokiona kama kutokuwa na utashi wa mdhamini mkuu, Marekani.

Bw Trump amekosoa vikali nia ya Ufaransa kutaka kutoza ushuru mkubwa kwa makampuni makubwa ya kiteknolojia ya Marekani. Utawala wa Trump tayari umetishia kutoza ushuru wa hadi 100% sawa na dola bilioni 2.4 za bidhaa kutoka Ufaransa ikiwa ni pamoja na Roquefort, yogurts na mvinyo.

Trump amesema rais wa Ufaransa, "amezikosea heshima" nchi zengine, mataifa wanachama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.