rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Boris Johnson

Imechapishwa • Imehaririwa

Boris Johnson: Nitaomba uchaguzi kama EU itachelewesha mchakato

media
Boris Johnson akizungumza katika Bunge Oktoba 19, 2019. ©UK Parliament/Jessica Taylor/Handout via REUTERS

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kushinikiza kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu iwapo Umoja wa Ulaya, utapendekeza nchi hiyo ijiondoe kwenye Umoja huo mwezi Januari mwaka 2020.


Mambo yameendelea kuwa magumu kwa Johnson baada ya wabunge kukataa mapendekezo yake ya kutaka mkataba mpya kujadiliwa haraka na kutiwa saini baada ya siku tatu.

Baada ya matokeo hayo, Boris amewalaumu wabunge na kusema wanachelewesha kwa makusudi mchakato wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

“Nasikitika kuwa wabunge wamepiga kura kuchelewesha kujiondoa kufikia Oktoba 31 na mkataba, sasa lazima serikali, iendelee kuweka mikakati ili kuwa tayari iwapo hakutakuwa na mkataba, lakini pia nitazungumza na wakuu wa Umoja wa Ulaya kusikia wanavyowaza, lakini, nisema kuwa sera yetu ni kuwa tusichelewe na tuondoke ifikapo tarehe 31”, amesema Waziri Mkuu wa Uingereza.

Sasa viongozi wa Umoja wa Ulaya wataamua iwapo wataiongezea muda Uingereza wa kujiondoa kwenye Umoja huo.