rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Boris Johnson

Imechapishwa • Imehaririwa

Boris Johnson: Nina imani kuwa wabunge wataunga mkono makubaliano yaliyofikiwa

media
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alitangaza Oktoba 17 kwamba amefikia "mkataba mpya" ulio bora wa "Brexit" na Umoja wa Ulaya. Reuters

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo Ijumaa anatarajiwa kuwasilisha mapendekezo mapya aliyokubaliana na viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu nchi yake kujiondoa kwenye Umoja huo, ifikapo mwisho wa mwezi huu.


Boris, alionekana mchovu baada ya mazungumzo ya saa nyingi na viongozi wenzake, amesema ana matumaini ya wabunge kuunga mkono makubaliano hayo.

Hata hivyo dalili zinaonesha kuwa huenda wabunge wakakataa maopendekezo hayo, na kumlazimu kisheria Waziri Mkuu Boris, kuahirisha kwa mara ya tatu nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja huo, suala ambalo amesema hatafanya.

Makubaliano hayo ni ushindi kwa Boris Johnson aliyeingia madarakani mwezi Julai uliopita akiahidi kuitoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya kuambatana na matokeo ya kura ya maoni ya mwaka 2016.

Hata hivyo makubaliano hayo yanaweza kupingwa yatakapowasilishwa mbele ya wabunge ili kuidhinishwa jumamosi inayokuja. Na ishara mbaya zimeshaanza kuonekana.

Sarafu ya Uingereza Pound imepungua thamani katika masoko ya hisa kutokana na wasiwasi kama bunge litayaidhinisha makubaliano hayo. Imepoteza % 0.34 ikilinganishwa na dola ya Marekani.Wakatai huo huo sarafu ya euro imepanda thamani kwa % 0.69.