Pata taarifa kuu
SWEDEN-POLAND-AUSTRIA-FASIHI

Tuzo za fasihi za Nobel zatunukiwa Olga Tokarczuk na Peter Handke

Mwaka mmoja baada ya kashfa ya unyanyasaji wa kingono na kutotolewa kwa tuzo yoyote, Taasisi ya tuzo nchini Sweden imewakabidhi Alhamisi hii Oktoba 10 Tuzo za Nobel kwa Fasihi mwaka 2018 na 2019 Olga Tokarczuk, raia wa Poland na Handman Handke, raia wa Austria.

Olga Tokarczuk na Peter Handke, washindi wa Tuzo za Fasihi mwaka 2018 na 2019.
Olga Tokarczuk na Peter Handke, washindi wa Tuzo za Fasihi mwaka 2018 na 2019. BARBARA GINDL, Beata ZAWREL / APA / REPORTER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tuzo mbili za Nobel katika fasihi zimetangazwa leo baada ya tuzo ya mwaka 2018 ya fasihi kuahirishwa kufuatia madai ya unyanyasaji kingono ambao ulitikisa taasisi hiyo ya tuzo nchini Sweden.

Jana Tuzo ya kemia ilikwenda kwa wanasayansi watatu kwa kazi yao ambayo imesababisha kupatikana kwa bateri ya lithium-ion.

Tuzo hiyo ilikwenda kwa wanasayansi wawili wa Uswisi na raia wa Canada na Marekani. Hadi sasa, tuzo tisa za Nobel zimetolewa wiki hii na wote waliopata tuzo hizo ni wanaume.

Tuzo ya amani ya Nobel inatarajiwa kutangazwa Ijumaa wiki hii na tuzo kuhusiana na masuala ya biashara itatangazwa Jumatatu wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.