rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Boris Johnson

Imechapishwa • Imehaririwa

Wabunge wa Uingereza wakataa pendekezo la Waziri Mkuu Boris Johnson

media
Wabunge wa Uingereza waamua hakuna uchaguzi wa mapema, na kupinga pendekezo la Waziri Mkuu Boris Johnson. PRU / AFP

Waziri Mkuu wa Uingereza amepata pigo mara mbili, baada ya wabunge kukataa pendekezo lake la kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini pia, kukataa mswada wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya bila ya mkataba.


Aidha, wabunge walio wengi, waliunga mkono pendekezo la nchi hiyo kupata kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na mkataba hata iwapo hili litafanyika baada ya Oktoiba 31, siku ya mwisho kujiondoa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Boris Johnson akijibu maswali ya wabunge, alimkosea kiongozi wa upinzani Jeremy Corbyn kwa kuwapotosha raia wa Uingereza, kuhusu suala hili.

“Kiongozi wa upinzani athibitishe kuwa, iwapo muswada wake utapitishwa,awarahusu wananchi wawe na uamuzi kwa kuwa na uchaguzi mkuu tarehe 15 mwezi Oktoba, bwana Spika, acha watu waamue kuhusu kile anachokofanyia watu kwenye nchi hii kwa kuwa na uchaguzi tarehe 15 mwezi Oktoba, “ amesema

Hata hivyo, wabunge wengi wakiongozwa na wale wa upinzani wanasema watakubali tu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu iwapo mkataba utapatikana.

Wabunge hao walikataa pia hoja ya Johnson ya kuiruhusu Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano mwezi ujao. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn, katika siku za nyuma alitaka uchaguzi mpya ufanyike, lakini chama chake kilijizuia katika kura ya Jumatano. Corbyn Amesema ataunga mkono uchaguzi mpya endapo tu uwezekano wa kuondoka bila ya makubalino utaondolewa

Jeremy Corbyn ni kiongozi wa upinzani anasema Waziri Mkuu Boris amekuwa mwongo.

“Amekuwa mwongo, tena mwoga sana na ana wasiwasi mwingi kuchunguzwa, “ amesema Jeremy Corbyn.