rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU Boris Johnson

Imechapishwa • Imehaririwa

Barnier: Msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu makubaliano ya Brexit hautobadilika

media
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mazungumzo ya namna ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, Michel Barnier, katika mkutano na waandishi wa habari, Brussels, Ubelgiji Novemba 19, 2018. 路透社。

Michel Barnier, mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mazungumzo ya namna ya Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, amesema Umoja huo hautabadilisha makubaliano yaliyokubaliwa hapo awali na Uingereza kuhusu kujiondoa kwake.


Wabunge nchini Uinegereza wanarejea bungeni wiki hii, wakiwa na lengo la kuzuia nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, bila ya mkataba.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anaamini kuwa bado kuna uwezekano wa kupatikana kwa makubaliano kati yake na viongozi wa Umoja wa Ulaya.

“Wabunge wakiendelea na msimamo wao wa kuzuia tusiondoke, bla mkataba, huenda ikawa hivyo, na kitu bora cha kufanya ni kuhakikisha kuwa, tunaendelea kungumza na mwenzetu wa Umoja wa Ulaya, kwa msisitizo na kutokata tamaa na hicvho ndichi tunachofanya”, “ amesema Bw Johson.

Kauli hii imekuja, wakati huu wabunge nchini Uingereza wanapotarajiwa kurejea bungeni wiki ijayo kujadili suala hili.

Bernier amesema, makubaliano ya kuuwacha mpaka wa Ireland Kaskazini kuwa, wazi, hata baada ya Uingereza kujiondoa mwisho wa mwezi ujao, hayawezi kubadililishwa licha ya wito kutoka kwa Waziri Mkuu Boris Johnson.