Pata taarifa kuu
ITALIA-USALAMA-SIASA

Italia yasalia bila serikali baada ya waziri mkuu kujiuzulu

Italia inaendelea kusalia bila serikali, siku moja baada ya waziri mkuu Giuseppe Conte kutangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo. Bw Conte amemnyooshea kidole cha lawama waziri wake wa mambo ya ndani Matteo Salvini kusababisha hali hiyo.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Contewakati akitoa hotuba mbele ya Bunge la Seneti, Agost 20 ambapo alitangaza kujiuzulu.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Contewakati akitoa hotuba mbele ya Bunge la Seneti, Agost 20 ambapo alitangaza kujiuzulu. AFP Photos/Andreas Solaro
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba aliyotoa mbele ya Bunge la Seneti jana Jumanne, Giuseppe Conte alitangaza kwamba anatarajia kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Sergio Mattarella, ambae ataamua iwapo anataka kuitisha uchaguzi wa mapema ama kujaribu kuunda muungano mpya wa serikali.

Bw Conte alimshtumu Waziri wake wa Mambo ya Ndani Matteo Salvini kwa "kutowajibika" kwa kusababisha mgogoro wa serikali ambao umeikabili nchi hiyo tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Hatua ya kujiuzulu ya Giuseppe ilikuja kufuatia uamuzi wa chama tawala cha Ligi kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani naye katika muungano huo unaounda serikali.

Kama Rais wa Italia, Matarrella anaweza kumuomba Conte kuendelea na wadhifa huo na kujaribu kutafuta mbadala wa wingi katika bunge, ama kukubali kujiuzulu kwake na kuangalia iwapo baadhi ya viongozi wengine wanaweza kuunda muungano mbadala wa uongozi. Ikishindikana, Mattarella anaweza kulivunja bunge , na kuiweka nchi hiyo katika uchaguzi wa mapema mwezi Oktoba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.