rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Italia Giuseppe Conte

Imechapishwa • Imehaririwa

Mgogoro wa kisiasa Italia: Hatma ya Giuseppe Conte kujulikana Jumanne hii

media
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte anatarajia leo kutoa hotuba mbele ya Bunge la Seneti, Jumanne 20 Agosti 2019. REUTERS/Alberto Lingria

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte anatarajiwa kutangaza kujiuzulu hivi leo, baada ya mshirika wake muhimu Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu, Matteo Salvini kujiondoa kwenye serikali ya muungano ambayo imeonekana kutoshirikiana katika masuala mbalimbali.


Suluhisho la mgogoro unaoendelea nchini Italia labda hautapatikana Jumanne hii, siku ambayo Waziri Mkuu Giuseppe Conte anatarajia kutoa hotuba mbele ya Bunge la Seneti. Lakini hotuba yake hii mbele ya Bunge la seneti ni kutaka kupima nguvu kuhusu vyama vinavyounga mkono uchaguzi wa mapema na vile vinavyopinga.

Hali ya kisiasa nchini Italia inakabiliwa na mvutano mkubwa.

Conte na Salvini waliounda serikali pamoja, wamekuwa wakitofautiana kuhusu sera mbalibali hasa kuhusu suala la wahamiaji, na hivyo kusababisha ugumu wa kushirikiana.

Uamuzi huu unaelezwa kuwa huenda ukasababisha Uchaguzi wa mapema katika taifa hilo ambalo kwa muda mrefu halijawahi kuwa na serikali inayomaliza muhula kamili.