rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Italia Giuseppe Conte

Imechapishwa • Imehaririwa

Italia: Wiki muhimu kwa hatma ya serikali ya Conte

media
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia Matteo Salvini katikakampeni ya uchaguzi Policoro (kusini), Agosti 10, 2019. © AFP

Italia inaanza Jumatatu wiki hii wiki yenye maamuzi kwa hatma ya serikali ya Giuseppe Conte, ambaye yuko hatarini kupoteza imani tangu kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia Matteo Salvini kutangaza kumng'oa kwenye wadhifa wake.


Makundi ya wabunge katika Bunge la Seneti yatakutana leo Jumatatu jioni lakini kuanzia asubuhi, vuguvugu la M5S, mshirika wa zamani ambaye Matteo Salvini alivunja uhusiano, litakuwa likihamasisha wanaharakati kadhaa kumuangusha kiongozi huo.

Yule ambaye wafuasi wake wanaomuita "Il Capitano" (Nahodha) atakusanya watu wake leo mchana.

Lengo lake: kuongeza shinikizo kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya serikali, kabla ya Agosti 20.

Mwishoni mwa wiki, Matteo Salvini aliendeleza kampeni yake aliyoita "safari ya fukwe" ili kupata kura nyingi kwa wakaazi wa Kusini mwa Italia.