Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-SIASA

Boris Johnson achukua mikoba ya May katika hali ya mvutano wa kujitoa EU

Waziri mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson, anatarajiwa kuanza kazi rasmi Jumatano wiki hii wakati atakapokutana na malkia Elizabeth wa pili kwa mazungumzo na kumkabidhi orodha ya baraza lake la mawaziri.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson.
Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Boris Johnson. REUTERS/Darren Staples
Matangazo ya kibiashara

Boris ambaye anachukua nafasi hii kutoka kwa mtangulizi wake Theresa May, anakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha nchi hiyo inajitoa kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31 mwaka huu, jambo ambalo hata yeye mwenyewe anajua litakuwa gumu kulitimiza.

Wakati huo huo washirika wakubwa wa Uingereza wamempongeza Boris Johnson baada ya kushinda.

Rais wa marekani Donald Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa anampongeza Boris Johnson kwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza. Trump ametangaza kuwa ni shabiki mkubwa wa Johnson.

Ursula von der Leyen kiongozi anayeingia madarakani kuwa mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya amempongeza Johnson kwa kusema anatarajia kuwa na uhusiano mzuri nae wa kikazi.

Wengine waliompongeza Johnson ni pamoja na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya wa majadiliano ya kujitoa Uingereza kutoka Umoja huo Michel Barnier , ambaye amesema Umoja huo unataka kufanya kazi na waziri mkuu mpya kuidhinisha makubaliano ya kujitoa na kufanikisha utaratibu mzuri wa Brexit.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.