rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza EU BREXIT

Imechapishwa • Imehaririwa

Uingereza: Wabunge waukataa mpango wa chama cha Labour kuhusu kujitoa EU

media
Picha inayoonesha bunge la Uingereza likiwa limejaa wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu, Theresa May. Tarehe 22 Mei 2019 HO / PRU / AFP

Wabunge nchini Uingereza wamekataa pendekezo la chama cha Labour kilichotaka wabunge wawe na uamuzi wa mwisho hatua ambayo ingepelekea nchi hiyo kujitoa bila ya makubaliano na umoja wa Ulaya.


Wabunge walipinga kwa kura 309 shida ya 298, ambapo ikiwa mpango wa Labour ungepitishwa basi nchi hiyo ingejitoa bila makubaliano ifikapo October 31 mwaka huu.

Matokeo ya kura hii yalipokelewa kwa shangwe na wabunge wa chama tawala cha Conservative kinachoongozwa na Waziri mkuu Theresa May.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn alisikika akiwaambia wabunge waliokuwa wakishangilia kuwa hawatakuwa wakishangilia ifikapo mwezi September.

Wabunge 10 wa chama cha Conservative ambao wamekuwa wakipinga mipango ya May, waliunga mkono pendekezo la chama cha Labour.

Hata hivyo pia wabunge 8 kutoka chama cha Labour ambao maeneo yao yalipiga kura kujitoa umoja wa Ulaya, walikaidi maelekezo ya chama kwa kupinga mapendekezo ya kiongozi wao.

“Hakuna makubaliano” kutamaanisha kuwa Uingereza itajitoa umoja wa Ulaya bila muafaka na kuamkia kesho yake nchi hiyo itakuwa haimo kwenye Soko la pamoja, ushuru wa forodha na kwenye taasisi za kisheria.

Kumekuwa na hofu kubwa ikiwa hakutakuwa na makubaliano ambapo biashara, usafi tu na mpaka wa Ireland itakuwa kikwazo kikubwa.