rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Donald Trump Theresa May Siasa EU

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump: Marekani kushirikiana na Uingereza kikamilifu hata baada ya kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya

media
Waziri Mkuu Theresa May na rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Hannah McKay/File Photo

Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi yake itashirikiana kikamilifu na Uingereza, katika masuala ya kibiashara hata baada ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya ifikapo mwezi Oktoba.


Trump ametoa hakikisho hilo siku ya Jumanne, wakati wa ziara yake ya siku ya pili nchini Uingereza, baada ua kukutana na Waziri Mkuu Bi.Theresa May.

Rais huyo wa Marekani, amemtania Waziri Mkuu May, kuwa aendelee kuwa madarakani ili ahakikishe kuwa anafanikisha ushirikiano imara kati ya nchi yake na Marekani.

“Naamini kuwa, tutakuwa na makubaliano mazuri ya kibiashara,” Trump amesema wakati wa mkutano na viongozi wa kibiahara kati ya mataifa hayo mawili.

Bi. May tayari amesema kuwa atajiuzulu siku ya Ijumaa, baada ya kupata shinikizo ya kuachia madaraka, kutokana na mzozo wa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Aidha, Trump amempongeza Waziri Mkuu May kwa kuonesha uongozi shupavu licha ya kuamua kuachia madaraka.

Hata hivyo, ziara ya Trump imekumbwa na maandamano kupinga ujio wake nchini Uiangereza huku waandamanaji wakikosoa sera zake ikiwa ni pamoja na kuwazuia wahamiaji kuingia nchini humo.

Maandamano hayo yalipangwa na Meya wa jiji la London, Sadiq Khan, na Trump akizungumzia hilo, amesema kuwa hakuona maandamano yoyote.

Ziara ya rais Trump inakamilika siku ya Jumatano, ambapo atashuhudia maadhimisho ya miaka 75, wakati wanajeshi wa Marekani na washirika wake walipoongoza operesheni dhidi ya jeshi la Ujerumani makabiliano ambayo yalimaliza vita vya pili vya dunia.