Pata taarifa kuu
UFARANSA-BURKINA FASO-USALAMA

Ufaransa yatoa heshima za mwisho kwa wanajeshi wawili waliouawa Sahel

Zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa wanajeshi wawili wa Ufaransa waliouawa usiku wa Mei 9 kuamkia Mei 10 wakati wa operesheni ya kuwaokoa mateka wawili wa Ufaransa waliokuwa wakishikiliwa nchini Burkina Faso, limefanyika leo Jumanne asubuhi kwenye makaburi ya mashujaa jijini Paris.

Majeneza ya Cédric Pierrepont na Alain Bertoncello kwenye makaburi ya mashujaa Paris, Mei 14, 2019.
Majeneza ya Cédric Pierrepont na Alain Bertoncello kwenye makaburi ya mashujaa Paris, Mei 14, 2019. REUTERS/Philippe Wojazer/Pool
Matangazo ya kibiashara

Viongozi mbalimbali wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Edouard Philippe, Waziri wa Mambo ya Ndani Christophe Castaner, Waziri wa Mambo ya Nje Jean-Yves Le Drian, Bruno Le Maire, Waziri wa Fedha na Nicole Belloubet, Waziri wa Sheria wamehudhuria sherehe hizo iliyofanyika kwenye makaburi ya mashujaa. Pia wamehudhuria sherehe hiyo kiongozi wa chama cha France Insoumise, Jean-Luc Mélenchon na waziri wa zamani François Bayrou. Nicolas Sarkozy na François Hollande pia wanahudhuria sherehe hiyo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongoza zoezi hilo kabla ya kutoa hotuba na kutoa taji la heshima kwa wanajeshi hao, Cedric Pierrepont na Alain Bertoncello.

Wanajeshi hao kutoka kikosi maalumu jeshi la Ufaransa cha Hubert waliuawa nchini Burkina Faso wakati wa operesheni ya kuwaokoa mateka wawaili wa Ufaransa.

Mateka hao wawili wa Ufaransa walitekwa mnamo Mei 1 mwaka huu katika Hifadhi ya Taifa ya Pendjari kaskazini mwa Benin ambako walipokuwa wakisafari, eneo ambako kunaripotiwa makundi kadhaa ya wanamgambo wa kijihadi.

Katika operesheni hiyo mateka wawili wa Ufaransa, raia mmoja wa Marekani na raia mmoja wa Korea Kusini waliokolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.